• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mongella apokea Vifaa tiba kutoka Mradi wa IMPACT kukabiliana janga la corona

Posted on: May 28th, 2020

Aga khan Development Network kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada (Global Affairs Canada) kupitia mradi wa Improving Access to Reproductive Maternal and Newborn Health (IMPACT)Mwanza wametoa vifaa kinga vya kukabiliana na  maambukizi ya Corona  vyenye thamani ya Million 572,272,498.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, Meneja Mradi wa IMPACT Mwanza Edna Selestine  amesema  fedha hizo zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba ,vitendea kazi pamoja na kuwezesha mafunzo ya watoa huduma za afya juu ya ugojwa huo pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii jinsi ya kuendelea kuelimisha jamii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi .

Anasema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa ushirikianao wa ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza hapahapa Nchini huku msaada huo ukiwalenga watoa huduma za afya na vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo.

Selestine amevitaja vifaa hivyo kuwa ni PPE,150 sets,Barakoa N95 750pcs, Chlorine tablets 100TB -300,surgical masks 35000pcs,Gloves examination,15000pairs na Gloves surgical 3500 pairs,vitakasa mikono 75lts,vitanda vya wagonjwa 30 na magodoro yake pamoja na mabegi 717 ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

 Aidha Agha Khan inapongeza juhudi zilizofanya na Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli  kwa namna alivyokabiliana na vieusi vya corona hadi kufikia hii leo ambapo maambukizi yamepungua kwa kiasi kikubwa.

"Tunatambua kupitia Wizara ya afya kuwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona yamepungua nchini pia tumehimizwa kuendeleza jitihada zote za kuendelea kujilinda, mradi wa IMPACT utaendelea kushirikiana na mkoa kila inapowezekana ili kuhakikisha gonjwa hili linatokomezwa kabisa na afya za wananchi zinaendelea kuwa salama" alisema Selestine.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza baada ya kupokea msaada huo amesema wamekuwa wabia na taasisi hiyo na wameweza kujenga majengo 28 katika vituo vya afya vya sehemu mbalimbali  kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto pia vitanda thelathini walivyotoa kwa ajili ya mapambano ya Corona amevigawa 10 Ilemela,Nyamagana 10 na Buchosa 10.

Vilevile aliendelea kuwasihi wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya wizara ya afya ,maombi,kutumia miti shamba iliyodhibitishwa sambamba na kupinga nyungu .

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti