• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mongella awaagiza ma DC kudhibiti mimba mashuleni

Posted on: October 16th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka viongozi wa Serikali mkoani  Mwanza kuiga mfano wa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda wa kuhakikisha wanawadhibiti watu wanaowapa ujauzito wanafunzi  wa kike na hivyo kukatisha ndoto za maisha kwa kushindwa kuhitimu elimu yao.

Alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda na Kamati yake ya ulinzi na usalama kwa hatua ambazo wamechukua za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu waliobainika kuwapa ujauzito watoto wa kike, akiwemo Mwalimu Peter Fred wa Shule ya Msingi Kifune wilayani humo ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwenda jela baada ya kubainika kuwa na hatia ya kumpatia ujauzito mwanafunzi.

“Nilipomuona Mwalimu yule kupitia kwenye mitandao na Televisheni  akiwa amepigwa pingu nilifurahi sana, ningekuwa na fedha ningemtumia DC wa Misungwi kwa kweli amefanya kazi kubwa sana," alisema  Mhe. Mongella na kuwataka wakuu wengine wa wilaya kuiga mambo mazuri yanayofanywa na uongozi wa wilaya ya Misungwi katika kudhibiti mimba mashuleni.

Aidha aliwataka wakuu wa wilaya za Ukerewe na Kwimba kuhakikisha wanadhibiti mimba mashuleni, pamoja na wilaya nyingine ili kuboresha elimu kwa mtoto wa kike.

“Kwimba hali ya utiaji wa mimba inatisha, utafikiri wilaya ina mpango maalum wa utiaji mimba kwa wanafunzi na DC mwanamke upo," alisema Mhe. Mongella.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Dkt. Philemoni Sengati alikiri kulishughulikia suala la mimba katika wilaya yake, lakini juhudi hizo zimekuwa zinakwamishwa na baadhi ya watendaji wa mahakama kushindwa kutoa haki kwa watuhumiwa wanaokuwa wamebainika kuwapatia ujauzito watoto wa kike.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti