• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AIHAKIKISHIA TUME HURU YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MWANZA

Posted on: August 9th, 2024

RC MTANDA AIHAKIKISHIA TUME HURU YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MWANZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameiambia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Mkoa wa Mwanza haujawahi kukwamisha shughuli au jambo lolote ambalo serikali imelipanga,  kwa maanaa hiyo pia hata uchaguzi Mkoani humo utakuwa wa amani na utulivu.

Mhe. Mtanda ameyasema hayo mapema leo Agosti 09, 2024 wakati alipokuwa akiipokea na kuikaribisha Mkoani Mwanza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyowasili Mkoani hapo kwa ajili ya mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema serikali ya Mkoa tayari imeshaanza  kuifanya kazi hiyo kwa kutoa elimu ya uchaguzi na upigaji kura kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ambayo imekuwa ikifanyika Mkoani humo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali vitakavyoainishwa ili warekebishe na kuandika taarifa zao.

"Tumejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, na kuanzia sasa niseme tu ofisi yangu itatoa ushirikiano wa kutosha mpaka pale uchaguzi utakapokamilika".

Naye Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amesema wamedhamiria kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na kwa Mkoa wa Mwanza wameanza na mkutano huo utakaowashirikisha wadau wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa, dini, asasi na makundi mbalimbali.

"Tume imeendelea na maandalizi mbalimbali ikiwemo ya kutoa elimu ya upigaji kura kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mikutano ya hadhara, pamoja na kutumia magari ya matangangazo". Amesema Mhe. Jaji Mwambelege.

Aidha Mwenyekiti wa Tume hiyo pia amemtaka Mkuu wa Mkoa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha elimu inasambaa zaidi kwa wadau wote kwa kuwa ana wasaidizi wengi hususani katika maeneo ya ngazi za chini za utawala.

Uboreshaji wa daftari la mpiga kura kwa Mkoa wa Mwanza unatarajiwa kuanza rasmi kuanzia 21 - 28 mwezi Agosti 2024.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti