• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AKABIDHI HATI ZA UMILIKI ARDHI ZILIZOKWAMA KWA TAKRIBANI MIAKA 10

Posted on: July 12th, 2024

RC MTANDA AKABIDHI HATI ZA UMILIKI ARDHI ZILIZOKWAMA KWA TAKRIBANI MIAKA 10


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo julai 12, 2024 amekabidhi hati za umiliki wa ardhi kwa wakazi watatu wa Manispaa ya Ilemela Wilayani Ilemela, waliodai kuhangaikia huduma hiyo kwa muda mrefu, baadhi yao takribani miaka kumi.

Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza hati hizo kuandaliwa ndani ya saa 24, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Idara ya Ardi ya  Manispaa ya Ilemela Julai 11, 2024, alipokukuta wananchi wengi wakiwa katika foleni ndefu kusubiri huduma na kuamua kuwasikiliza.

Idadi kubwa ya wananchi ilieleza kero ya kuzungushwa na watoa huduma kwa muda mrefu, akamuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa kuandaa hati hizo kwa waliokidhi vigezo haraka iwezekanavyo, ambapo mapema leo amerudi tena wilayani huko kuwakabidhi nyaraka hizo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hati ya umiliki wa ardhi Bi. Immaculata Tenga ambaye pia ni mjane aliyetumia zaidi ya mika tisa kuisaka hati hiyo bila mafanikio, amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa na kusema haikuwa rahisi kwani amekuwa akizungushwa mara kadhaa katika ofisi hizo za ardhi na anaona ni kama ndoto kukabidhiwa hati hiyo siku ya leo.

"Ninakushukuru sana Mkuu wa Mkoa, wewe ni baba katika Mkoa huu, umenisaidia sana nimefanikiwa kuipata hati yangu ambayo nimeisotea kuipata kwa muda mirefu". Bi. Tenga.

Kwa upamde wake Bi. Anna Mbwambo ambaye pia ni majane amesema amesumbuliwa kwa muda murefu na amekuwa akitumia gharama kubwa kwa safari kutoka Dar es Salaam kuja Mkoani Mwanza kufuatilia hati hizo.

"Kwa sasa ninaishi Dar es Salaam nimekuwa na safari za kila wakati kufuatilia hati hii, naona ni kama muujiza nimeipata ndani ya saa 24, Ninakushuru sana Mkuu wa Mkoa". Amesema Bi. Mbwambo.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi hati hizo Mkuu wa Mkoa amesema wema ni akiba na kuwataka watumishi kuwatendea vyema wananchi kwani thawabu zitapatikana hapa duniani na hata kesho akhera, hakuna haja ya kuwacheleweshea wananchi haki zao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti