• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AKABIDHIWA OFISI RASMI, AAHIDI UTUMISHI WA USHIRIKIANO

Posted on: April 6th, 2024

RC MTANDA AKABIDHIWA OFISI RASMI, AAHIDI UTUMISHI WA USHIRIKIANO


Kufuatia Mabadiliko aliyoyafanya Rais Samia siku za karibuni, leo Aprili 06, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mohamed Mtanda amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekua Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla baada ya kuhamishiwa kutoka Mkoa wa Mara.

Akiongea na hadhara baada ya makabidhiano hayo Mhe. Mtanda amesema katika uongozi wake ataendeleza yale yote yaliyoasisiwa na mtangulizi wake na kwamba anaamini kwenye ushirikiano hivyo anautegemea kwa viongozi wote naye atashirikiana nao kwa dhati.

Naye, aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhe. CPA Amos Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumuamini na baada ya kumtoa kwenye Mkoa wa Mwanza amemteua kwenda kuhudumu kwenye nafasi ya Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo.

Aidha, ameipongeza Serikali kwa miradi lukuki ya kimkakati hususani Reli ya SGR, Daraja la Kigongo-Busisi, Ukarabati wa Meli ya mizigo pamoja na ujenzi wa Meli ya kisasa ya MV Mwanza pamoja na uboreshaji wa uwanja wa ndege kuwa wa Kimataifa kwamba ukamilifu wa miradi hiyo utaifungua zaidi Mwanza kiuchumi.

Aidha, amewashukuru watumishi na viongozi wote alioshirikiana nao katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani amewasifu kwa kutembea naye sambamba vijijini ambako muda mrefu alifika kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi katika kuwasikiliza na kutatua migogoro inayowakabili.

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na Kamati ya Usalama Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu Tawala, Kamati ya amani, Shirikisho la vyama la wenye ulemavu, viongozi wa vyama vya siasa, wazee wa Mkoa wa Mwanza, Watemi na Machifu, Kamati Tendaji ya Pamba Jiji FC, Chuo cha SAUT, Watumishi wa RS pamoja na Wafanyabiashara.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti