• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI, VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA, AHIMIZA ULIPAJI KODI NA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Posted on: May 9th, 2024

RC MTANDA AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI, VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA, AHIMIZA ULIPAJI KODI NA HUDUMA BORA KWA WANANCHI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Mei 9, 2024 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amekutana kwa nyakati tofauti na Wakuu wa Taasisi za Umma, viongozi wa Wamachinga na viongozi wa Wafanyabiashara kwa lengo la kufahamiana na kufahamu shughuli zao.

Akianza mkutano huo na Wakuu wa Taasisi za Umma, Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha kutambua wajibu wao kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati.

"Rais Samia ameonesha kwa vitendo anavyowapigania maendeleo wananchi,na sisi tunavyotoa huduma bora wananchi watazidi kuifurahia Serikali yao",Mkuu wa Mkoa

Amewataka viongozi hao kutekeleza wajibu wao kwa kuimarisha nidhamu ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa upendo na kuheshimiana na kuepuka aina yoyote ya unyanyasaji au kupokea rushwa kutoka kwa wananchi

Amesema yupo mbioni kuanza ziara kutembelea maeneo yote mkoani humo ili kujionea maendeleo ya wananchi na changamoto zinazowakabili.

"Ndugu viongozi mkutano huu siyo wa kusikiliza changamoto zenu na kuzitolea majibu hapa la hasha! lengo ni kufahamiana na kujua shughuli zenu mkitambua sina muda mrefu tangu nihamishiwe hapa nikitokea Mara,"amesema Mhe.Mtanda.

Katika mkutano wake wa pili na viongozi wa Wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga,Mhe.Mtanda amewaahidi kuwatembelea maeneo yao ili kujionea hali halisi kabla ya kuchukua maamuzi yenye malengo ya kuboresha shughuli zao.

"Mkoa wa Mwanza una jumla ya masoko 50 yenye wafanyabiashara wadogo 19,969 ambao wapo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza,"Yesaya Sikindeni,Afisa Biashara Mkoa.

"Nimesikia changamoto zenu uzuri nina uzoefu wa kutosha na kero zinazo wasumbua,nimesikia taarifa fupi kutoka kwa Afisa biashara ikiwemo hali ya masoko na mazingira yenu,kuweni na utulivu na fanyeni shughuli zenu kwa kuheshimu maelekezo mliyopewa na Serikali,"Mkuu wa Mkoa

Akimalizia mkutano huo na viongozi wa Wafanyabiashara wakubwa ,mkuu huyo wa Mkoa amebainisha anatambua mchango wao katika pato la Taifa na kusisitiza kuendelea kushirikiana katika ujenzi wa Taifa.

"Tujengeni nidhamu ya ulipaji kodi kwa uungwana na Serikali imeweka bayana masikilizano baina ya mamlaka za kodi na wafanyabiashara hakuna mtu wa kukufungia biashara yako," Mhe.Mtanda.

Amewakumbusha pia Mamlaka za usimamizi wa kodi kuwacha kutumia lugha za vitisho au aina yoyote ya utovu wa nidhamu badala yake kufanya kazi zao kwa kufuata Sheria na kanuni zilizopo huku wakiweka mazingira rafiki na wafanyabiashara.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti