RC MTANDA AMPOKEA NA KUFANYA MAZUNGUMZO OFISINI KWAKE NA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI DKT.ANNA MAKAKALA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda mapema leo Juni 03 2024, amempokea Ofisini kwake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna P. Makakala ambaye amewasili Mkoani Mwanza kwa ajili ya zoezi la uvalishaji wa nishani kwa maafisa na Askari wa Uhamiaji Kanda ya Ziwa.



