• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA MTOTO WA KATIBU WAKE

Posted on: November 16th, 2024

RC MTANDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA MTOTO WA KATIBU WAKE


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Novemba 16, 2024 amewaongoza watumishi wa Ofisi yake na waombolezaji katika mazishi ya mtoto wa katibu wake Faith Matia Levi.

Akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Imani, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Christopher Ngubiagai  amewataka familia ya Bw.Matia Levi kusimamia imara na kumtumainia Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kipenzi chao.

Amesema siku zote kifo huwa hakizoeleki na kinakuja pasipo kutarajia hivyo wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

"Nawashukuru wote tulioguswa na msiba huu tangu taarifa ilipotolewa na kuwafariji wafiwa, tuendelee kuwatia nguvu na moyo wafiwa katika muda huu wa maombolezo", DC Ngubiagai.

Awali akitoa mahubiri wakati wa ibada ya mazishi mchungaji wa kanisa hilo amesema mwanadamu hana sababu ya kuwa na hofu ya kifo kwani siku yake ya kurejea kwa Mungu ipo hivyo wajibu wake ni kuishi kwa furaha kwa kumtumainia Mungu.

"Leo wafiwa wana huzuni ya kumpoteza mtoto wao, lakini hili ni fumbo kwa Mungu la kumtwaa Faith akiwa na umri mdogo ili akapate nafasi zaidi ya kutuombea na sisi tunaondelea na zawadi hii ya uhai", Mchungaji Mahisa.

Akitoa historia fupi ya marehemu, mama mdogo wa marehemu amesema Faith alizaliwa Februari

06, 2019 hospitali ya Kanda ya Bugando akiwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa ambaye hadi mauti yanamkuta hospitali ya Mkoa ya rufaa ya Sekou Toure Novemba 13, a024 alikuwa darasa la awali shule ya msingi Nyakahoja huku akiwa na ndoto za kuwa daktari wa hospitali ya Sekou Toure.

Salamu mbalimbali za rambi rambi zimetolewa kwa wafiwa ikiwemo Ofisi binafsi ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa, Taasisi za Umma,Taasisi za dini, umoja wa wabunge Mkoa wa Mwanza na makundi mengine mbalimbali yanayoshirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza

Marehemu Faith Matia amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele alasiri ya Novemba 16, 2024 Kisesa wilayani Magu ambako ni eneo la familia.

Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti