• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA, AMSHUKURU RAIS SAMIA

Posted on: May 17th, 2024

RC MTANDA ARIDHISHWA NA UJENZI WA  MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA, AMSHUKURU RAIS SAMIA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo ameendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi ya kimkakati akiwa wilayani Nyamagana ameanzia kuona ujenzi wa Soko kuu lililogharimu zaidi ya shs bilioni 23 na kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi ya miradi mbalimbali Mkoani humo, huku akimuhimiza mkandarasi Mohamed Builders kulikamilisha mapema.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua iliyofikia soko hilo ya 94% kabla ya kukamilika ni nzuri na tayari pesa iliyobaki shs bilioni tatu imeshatolewa na Serikali ili Mkandarasi akamilishe na wafanyabiashara waanze kufanya kazi.

"Tuendelee kumshukuru na kumuombea Rais wetu Samia Suluhu Hassan wakati anaingia  madarakani soko hili lilikuwa hatua ya ujenzi asilimia 40  na Mkandarasi akiwa amelipwa 30%,lakini Rais akaongeza asilimia 60 ya malipo yake na sasa tunaona soko limebakiza asilimia 6 kabla ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi licha ya kupitia changamoto mbalimbali,asante sana Mhe.Rais,"Mkuu wa Mkoa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu kutoka Halmashauri ya Jiji,Mussa Joram amebainisha soko hilo likikamilika wanatarajia kukusanya mapato ya shs bilioni 3.5 kwa mwaka.

Mkuu wa Mkoa akiwa kwenye mradi wa Hoteli ya nyota 5 inayojengwa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF wenye gharama ya sh bilioni 123 eneo la Capri Point,Mtanda amezihimiza Taasisi zote zinazohusika ikiwemo Tanesco na Mwauwasa kutoa ushirikano ili mradi huo uliofika asilimia 60 ya ujenzi ukamilike kama ulivyokusudiwa Disemba mwaka huu.

Mtanda amesema miradi kama hiyo inahitajika Mkoani humo kutokana na ujenzi wa uwanja wa ndege unaoendelea kufanyika ili uwe wa Kimataifa utaleta wageni wengi hasa watalii.

"Mhe Mkuu wa Mkoa Hoteli hii sasa hivi ipo asilimia 60 ya ujenzi,huduma kamili tunarajia kuanza kutoa Machi mwakani ikiwa na vyumba 195 vya kulala kikiwemo chenye hadhi ya Rais",Emmanuel Kahensa,Meneja NSSF Mwanza.

Mkuu huyo wa Mkoa alipofika kwenye mradi wa Meli ya Mv Mwanza inayojengwa eneo la Mwanza South amewapongeza Kampuni ya huduma za Meli MSCL  kwa kuwa na chombo hicho cha kisasa na kinachoongoza kwa ukubwa ukanda huu wa Afrika eneo la maziwa.

"Huu ni mradi mkubwa sana ambao utachochea uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla,Mwanza ni Mkoa uliopo kimkakati eneo la nchi za maziwa makuu,Meli hii ikianza kutoa huduma kupitia nchi za Uganda na Kenya tutazidi kuimarika kiuchumi",Mkuu wa Mkoa

Amesema Meli hiyo itabeba abiria 1200 na tani ya mizigo 400 yakiwemo magari madogo 20 na Malori 3,ni huduma kubwa na ya kisasa ambayo Serikali imegharamia kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.

"Meli hii imeigharimu Serikali shs bilioni 123 na Mkandarasi GAS ENTEC ameshalipwa fedha kwa asilimia 91 tunarajia mwishoni mwa mwezi huu tukabidhiwe Meli hii,"Erick Hamis,Mkurugenzi,MSCL

Mhe.Mtanda amekamilisha ziara yake siku ya leo kwa kukagua mradi wa chanzo cha maji eneo Butimba wenye gharama ya zaidi ya shs bilioni 71 na hapo amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maji na kuwataka wananchi kuilinda miundombinu ya rasilimali hiyo.

Mtanda amewakumbusha wananchi kujenga tabia ya kulipa ankara za maji kwa wakati ili Serikali izidi kupata fedha na kuwaongezea huduma bora.

"Hongera sana Nelly Msuya kwa hatua hii,mnatekeleza vizuri ilani ya CCM ya kumpatia huduma bora ya maji safi na salama mwananchi.

"Mhe.Mkuu wa Mkoa MWAUWASA tupo mbioni kujenga Matenki makubwa 5 yatakayokuwa na ujazo wa maji lita milioni 31 maeneo ya Fumagila,Buhongwa,Nyamazobe,Kisesa na Usagara lengo ni kuwapatia huduma endelevu ya maji wakazi wa maeneo hayo,"Nelly Msuya,Mkurugenzi MWAUWASA

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti