• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATOA MUDA WA MIEZI MITATU WANAODAIWA 5% YA MIKOPO YA HALMASHAURI KUZIREJESHA

Posted on: June 28th, 2024

RC MTANDA ATOA MUDA WA MIEZI MITATU WANAODAIWA 5% YA MIKOPO YA HALMASHAURI KUZIREJESHA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wanachi wote wanaodaiwa marejesho ya mikopo waliyochukua kutoka Halmashauri ya wilaya ya Magu zaidi ya mil. 148 kuhakikisha wanazirejesha fedha hizo ndani ya miezi mitatu ili na wananchi wengine wenye sifa na vigezo waweze kunufaika.

Mhe. Mtanda ametoa kauli hiyo mapema leo Juni 28, 2024 alipokuwa akizungumza katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG) za mwaka 2022/2023 na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa kupata hati inayoridhisha na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

"Mkopo huu sio hisani na wala sio mgao wa kula, wale wote waliopitiliza muda wa marejesho watafutwe wabanwe wazilipe ili tuweze kuwakopesha wanawake wengine, nchi hii ina wahitaji wengi".Mtanda

Mkuu huyo wa Mkoa amesema nia ya Serikali kutoa 5% ya fedha ya mapato ya ndani za  Halmashauri ni kuwasaidia wanawake katika harakati za kupambana na kujikomboa na umaskini kwa kuwawezesha kutumia fedha hizo katika kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha Mhe. Mtanda ameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha wanamaliza hoja 11 zilizobakia kwa wakati na kusema kuwa ameridhishwa na namna walivyojipanga kuzimaliza hoja hizo. Kadhalika amewataka kuwasilisha Mkoani mpango kazi wa namna ya kuzimaliza hoja hizo ifikapo tmJunu 29,2024 mwaka huu ili mpango kazi huo uunganishwe na utumwe Wizarani TAMISEMI.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mhe. Simon Pandarume amesema wao kama Halmashauri wana ushirikiano wa kutosha kwani wamefanikiwa kuongeza mapato ya ndani kutoka sh. bil. 2.4 na kufikia bil. 4.4 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Tumefungua Shule nyingi kwa mapato ya ndani, 19 mpya za Sekondari na 7 za Msingi kwa miaka minne, tumepeleka pia fedha nyingi kwenye zahanati, nyumba za watumishi, wakiwemo waalimu". Amesema Mhe. Pandarume.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti