• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATOA MWEZI MMOJA KWA TAKUKURU KUICHUNGUZA KAMPUNI YA UJENZI MISUNGWI

Posted on: June 17th, 2025

RC MTANDA ATOA MWEZI MMOJA KWA TAKUKURU KUICHUNGUZA KAMPUNI YA UJENZI MISUNGWI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa muda wa mwezi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuingia kazini kuichunguza Kampuni ya UJENZI MISUNGWI inayomilikiwa na Halmashauri kwa kushindwa kuandaa Taarifa yake hali iliyopelekea kuzalishwa kwa hoja na miradi kushindwa kutekelezwa.

Mhe. Mtanda ametoa tamko hilo mapema leo wakati akizungumza katika Baraza la Madiwani kuhusu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na kuwataka TAKUKURU kuharakisha uchunguzi huo ili hatua stahiki ziweze kufuatwa.

Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa pia ameagiza kurudishwa kwa shilingi milioni 46 zilizotolewa kama mkopo kupitia kundi la Vijana, Aidha ametoa tahadhari kuwa wale wote waliochukua fedha hizo wazirudishe kwa wakati na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoshindwa kufanya marejesho ya fedha hizo.

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wawekezaji waliopatiwa viwanja na Halmashauri ambao wameshindwa kuviendeleza viwanja hivyo kuvirudisha mara moja katika umiliki wa Halmashauri ili wapewe wenye uwezo wa kuvuendeleza.

Zaidi ya hayo, Mkuu wa Mkoa ameitaka Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya Wataalamu na Baraza la Madiwani ili kutokuzalisha hoja za ukaguzi.

Akiwasilisha Taarifa yake, Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi CPA Andrew Ndaba amesema katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2023/2024, Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi zilikaguliwa na Ofisi ya Mdhubiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, na taarifa ya ukaguzi imebainisha kuwa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi ilipata hati inayoridhisha (Unqualified Opinion).

Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ilikuwa na Jumla ya Hoja 41. Kati ya hizo hoja za miaka ya nyuma zilikuwa 14 na hoja za mwaka wa fedha 2023/2024 zilikuwa 36, zilizofungwa baada ya uhakiki ni 12 hivyo hoja zilizobaki hadi sasa ni 17. Amesema CPA Ndaba.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti