• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATOA WITO KWA WANANCHI KUITUMIA VYEMA SIKU YA MWISHO KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Posted on: August 27th, 2024

RC MTANDA ATOA WITO KWA WANANCHI KUITUMIA VYEMA SIKU YA MWISHO KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kutumia vyema siku ya mwisho ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo mapema leo  Agosti 27, 2024 wakati akiboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la wapiga kura katika kituo cha Isamilo Kaskazini kilichopo kata ya Isamilo Wilayani Nyamagana.

Amesema, kuwa na kitambulisho cha kupigia kura ndio silaha ya demokrasia kwani kitampa mwananchi fursa ya kuchagua kiongozi amtakaye kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.

Aidha, amebainisha kuwa muitikio wa wananchi mkoani humo kwenye kujiandikisha ni mkubwa na akafafanua kwamba mwananchi atakayefika kwenye foleni ya kujiandikisha kabla ya muda wa kufunga vituo atapata haki hiyo.

Halikadhalika, amebainisha kuwa zoezi hilo ni la muda mfupi sana kwani ndani ya dakika tatu mwananchi anakua ameshapata kitambulisho cha kupigia kura na anaondoka kwenda kuendelea na shughuli zake.

Vilevile, ametumia wasaa huo kutoa wito kwa wananchi mkoani humo kujituma katika shughuli halali za kujitafutia kipato badala ya kukaa kwenye vijiwe kubishana na kuzungumza mambo yasiyo na msingi kwani fursa zipo nyingi kinachotakiwa ni kujibidiisha tu.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Mwanza lilianza  Agosti 21,2024 na linatarajiwa kukamilika leo Agosti 27, 2024 saa 12 jioni ikiwa na kaulimbiu isemayo "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti