• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AUPOKEA MSAFARA WA BALOZI KUTOKA BURUNDI

Posted on: July 13th, 2024

RC MTANDA AUPOKEA MSAFARA WA BALOZI KUTOKA BURUNDI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Julai 13, 2024 ameupokea Ofisini kwake msafara wa Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Balozi Gelasius Byakanwa pamoja na wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu kutoka mjini Bujumbura nchini Burundi.

Ugeni huo umewasili Mkoani Mwanza kwa lengo la kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao Mhe. Matanda amesema Serikali ya Tanzania chini ya Mhe. Rais Samia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Burundi chini ya Mhe. Rais Ndayishimiye.

Aidha, Mtanda amewataka vijana hao kuhakikisha wanalinda amani waliyonayo kwani madhara na athari za uharibifu wa amani hiyo tayari wanazijua, hivyo amewataka kuiendeleza amani waliyonayo kwa kutokukubali kutumika kuvunja amani yao.

"Ukishashiba amani unaanza kuwaza kuharibu amani, ni lazima tujenge utaratibu wa kuthamini amani, nchi kama Burundi mna uzoefu mkubwa wa amani ni nini". Mhe. Mtanda.

Ukiwa katika nchi yako huwezi kuona thamani ya nchi uliyonayo ila ukiwa ugenini ambapo ni uhamishoni ndio utakapoona thamani ya nchi yako, Warundi lazima mjivunie Urundi wenu kwa sababu ndio thamani yenu. Ameongeza Mhe. Mtanda.

Kadhalika, Mhe. Mtanda amewasihi Wanafunzi na walimu hao kuhakikisha wanendelea kudumisha umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuidumisha na kuiendeleza lugha ya kiswahili ili pia kiweze kukidhi vigezo vya kutumika katika nyanja nzima ya teknolojia.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Burundi , Mhe. Balozi Gelasius  Byakanwa amesema wao kama ubalozi waliamua kwa juhudi zote kuikuza na kuisambaza lugha ya kiswahili na wakaona waje na utaratibu wa kushindanisha wanafunzi wa vyuo vikuu katika uandishi wa insha mjini Bunjura, lengo likiwa ni kuhakikisha wanakikuza na kukiendeleza lugha adhimu ya kiswahili.

Aidha Mhe. Balozi Byakanwa amesema wako Mkoani Mwanza kujionea yale mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati kama vile mradi wa daraja la kigongo - Busisi, ujenzi wa Neli kubwa ya Mv. Mwanza Hapa  Kazi Tu.

"Nina imani hawa vijana watakua mabalozi wazuri wa lugha ya kiswahili na yale tuliyoyashuhudia hapa Mwanza na hawa wataleta watu wengi zaidi, lakini pia hawa tunaweza kuwaita wavuvi ambao watakwenda kuvua wengi zaidi waje kutalii Mkoani Mwanza".

Vijana hawa jana wameshuhudia kwa macho yao namna daraja lilivyojengwa juu ya maji, ujenzi wa Meli ya Mv. Mwanza Hapa Kazi Tu na wengine pia walikua hawajawahi kupanda hata meli hivyo wamepanda hapa Mwanza, nikuhakikishie RC, hawa watakwenda kuutangaza vyema Mkoa huu wa Mwanza. Ameongeza Mhe. Balozi Byakanwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti