• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AWATAKA BODABODA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Posted on: November 9th, 2024

RC MTANDA AWATAKA BODABODA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka maafisa usafirishaji wa pikipiki za abiria (Bodaboda) Mkoani humo kufuata sheria za usalama wa barabarani ili kujiepusha wao na abiria wanaowabeba na ajali za barabarani.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo  Novemba 09 2024 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza wakati akifungua Mkutano mkuu wa jumuiya hiyo ambapo wanakwenda kuchagua viongozi katika ngazi za kanda, mkoa na wilaya wa kundi hilo.

"Nawasihi sana twendeni tushirikiane kuzuia ajali, tutambue kwanza kuwa hatuvai kofia ngumu (helmet)kwa ajili ya kumfurahisha askari wa barabarani (trafiki) bali ni kwa faida yetu wenyewe." Mhe. Mtanda.

Aidha, amewataka kuwa walinzi wa amani baina yao kwa kuhakikisha kila mmoja anamfahamu mwenzake na anapoona mwenendo mbaya unaoashiria uhalifu basi mara moja atoe taarifa katika uongozi wa serikali ya mtaa.

Ametumia wasaa huo kuwataka pia kuacha tabia za kuchagua viongozi ambao ni wababe na wabishi kwa ajili ya kuwaandaa kubishana na viongozi wa wilaya bali wakachague viongozi waadilifu  ili wawasaidie siku za usoni.

"Twendenu tukashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya jumatano  Novemba 27, 2024 na pia tunaimarishe usalama katika kipindi chote cha uchaguzi huu." Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Mhe. Mtanda ameichangia jumuiya hiyo inayoendesha shughuli zao na kaulimbiu isemayo 'Bodaboda Usafiri Salama' Tshs. 500,000 kwa ajili ya kuwaongezea nguvu katika majukumu yao

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti