• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA: MALEZI YA MABAVU CHANZO CHA KUMJENGEA HOFU MTOTO

Posted on: June 16th, 2024

RC MTANDA: MALEZI YA MABAVU CHANZO CHA KUMJENGEA HOFU MTOTO


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw.Balandya Elikana  amewataka Wazazi na Walezi kuzingatia wajibu wa malezi bora kwa watoto maana  yana mchango mkubwa  katika kuwajengea maadili mema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Juni 16,2024 kwenye ukumbi wa Gold Crest katika siku ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,Balandya amebainisha malezi sahihi ni kujenga urafiki na ukaribu na mtoto na siyo vinginevyo.

Mtendaji huyo wa Mkoa amesema Wazazi wengi wanaamini kuwa matumizi ya nguvu na ukali (malezi ya mabavu) ndio njia sahihi ya malezi kwa watoto ambapo amesema madhara ya njia hiyo ni kumjengea hofu mtoto hivyo kuondoa dhana ya uthubutu katika ubunifu.

"Pia matumizi ya nguvu yanaweza kuudhuru mwili wa mtoto, vile vile mtoto anaweza kuathirika kisaikolojia madhara ambayo yanaweza kudumu maisha yake yote".amesisitiza Balandya

Aidha  ametoa rai kwa wazazi kuachana na malezi ya kuwadekeza watoto kwa kuwapatia chochote wanachohitaji hata kama sio muhimu ambapo amesema madhara yake ni kumjengea mtoto mtazamo kuwa kila kitu kinapatikana kirahisi.

"Hisia hizo zinaweza kuendelea katika maisha yake yote, kujenga familia na taifa la kuamini katika njia za mkato na sio kupata kwa jasho - Tunashuhudia wizi na ubadhilifu ili kutimiza azma hiyo".

Akisoma risala ya watoto wa Mkoa wa Mwanza kwa mgeni rasmi, mtoto Josephine Bakita amesema wanaipongeza Serikali katika kuhakikisha watoto wanapata haki za msingi hususani elimu kwani imefanikiwa kujenga shule nyingi nchini na kuweka mfumo wa elimu bila malipo kwa Shule zote, watoto wengi wenye mahitaji maalumu na wasio na mahitaji maalumu wanapata elimu sawa.

Sambamba na hayo pia amewasilisha changamoto zinazowakabili watoto amesema wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa miundombinu rafiki kwa watoto wenye mahitaji maalumu shuleni, upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia pamoja na uhaba wa Walimu wenye taaluma ya elimu jumuishi.

Akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa  Balandya amesema kuwa Serikali Mkoani Mwanza kwa kushirikiana na sekta binafsi wamekuwa wakishirikiana katika upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya kujifunzia hivyo kama kuna mtoto yoyote mwenye uhitaji basi afike Ofisi ya Mkuu wa Mkoa aweze kupatiwa vifaa hivyo, aidha suala la uhaba wa walimu na miundombinu rafiki amesema ameyachukua kwa ajili ya utekelezaji.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2024 ni "Elimu Jumuishi kwa Watoto Izingatie Maarifa, Maadili na Stadi za Kazi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti