• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA WATAKA WAZEE KUWA MABALOZI WA MAADILI MEMA

Posted on: June 7th, 2024

RC MTANDA WATAKA WAZEE KUWA MABALOZI WA MAADILI MEMA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wazee kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuelimisha vijana kuwa na Maadili mema na kuachana na tabia hasi zinazosababisha kuwepo na mmomonyoko wa maadili.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo wilayani Misungwi wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo ambao kwa kauli moja wameonesha imani kubwa kwa Rais Samia katika kuliletea Taifa maendeleo.

"Ni lazima tujenge familia bora na imara, tunapaswa kujiandaa na kustaafu mapema na siyo kuongeza mke bali tunapaswa kujiandaa na uzee kwa kujiandalia mahali pa kuishi." Mhe. Mtanda.

Amebainisha kuwa fidia zinazolipwa kwa wananchi wa Fela wanaopisha mradi wa SGR ni ishara ya hatua kubwa zaidi ya maendeleo inayokuja kwa wananchi wa

Misungwi hivyo ni lazima kujiandaa kunufaika nazo kwa kuwekeza.

"Mradi wa kimkakati wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 700 (Daraja la Kigongo Busisi) unakaribia kukamilika, ndani ya miezi 3 daraja letu linakamilika na kupitia takwimu za abiria wanaotumia kivuko inaonesha kuna watu wengi sana wanatumia barabara hiyo, tujiandae kunufaika," Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Vilevile, ameutaja mradi wa Ujazilizi wa Umeme wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 8 na kuna megawati za umeme zaidi ya 80 lakini unaotumika ni umeme kidogo tu na kwamba zaidi ya Bilioni 11 zimekuja kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme (REA).

"Serikali inasisitiza malezi bora ya watoto kuanzia unyonyeshaji hadi makuzi na kuwapatia elimu bora ili baadaye waweze kuwatunza wazee wao na Serikali inawahakikishia usalama popote walipo hata walio kwenye vituo vya malezi maalum na wanufaika wa mradi wa uhaulishaji fedha chini ya TASAF wataendelea kunufaika kwa mujibu wa taratibu." Mtanda.

Mkuu wa Wilaya ya Misungi Mhe. Johari Samizi amesema tatizo la maji kwenye kata ya Usagara linakwenda kumalizika hivi karibuni kwani tayari kuna mkandarasi anayejenga mradi wa maji mkubwa kwenye kata hiyo yenye vijiji vinne na akatoa agizo kwa watumishi wa afya kuwajali wazee bila kuchoka.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilaya ya Misungwi Josiah Gambishi amesema anajivunia umoja na ushirikiano walionao ndani ya wilaya hiyo unaochagizwa na uongozi bora wa Mkuu wa Wilaya hiyo na kwa kauli moja wameonesha imani kwa uongozi wa Rais Samia na kusema anatosha kuongoza nchi kwa miaka 5 mingine.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti