• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mwanza aagiza Halmashauri zote kutenga na kupeleka fedha za Miradi ya Lishe kwa wakati

Posted on: June 13th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe, Mhandisi Robert Gabriel ameziagiza Halmashauri mkoani humo kutenga na kupeleka fedha za miradi ya Lishe kwa wakati ili kutekeleza Afua za Lishe na kuweza kusaidia jamii kuwa na afya bora na kuondoa Udumavu kwa watoto.


Mhandisi Robert Gabriel amesema hayo leo Juni 13, 2022 wakati akifungua kikao cha kupitia utekelezaji wa mkataba wa lishe, kupata taarifa ya Kampeni ya Chanjo ya Polio na Maandalizi ya kampeni ya Chanjo ya Uviko 19 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Aidha, amewataka Maafisa Lishe kutoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la Afua za Lishe kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya kila wiki zikionesha mafanikio na changamoto  kwenye wiki husika ili kwa kushirikiana na Halmashauri waweze kufanikisha kampeni hiyo.


Kuhusu utekelezaji wa kampeni ya Chanjo ya Ugonjwa wa Polio Mhe Mkuu wa Mkoa amewapongeza wadau na viongozi kwa kufanikisha Chanjo hiyo kwa watoto zoezi ambalo yeye mwenyewe ndiye alizindua rasmi wilayani Ukerewe.

Vilevile, Chanjo ya Uviko 19 imeonesha Ukerewe kuongoza kwa idadi ya watu waliochanjwa hadi sasa kwa zaidi ya asilimia 65 na ndipo Mkuu wa Mkoa aliwapongeza na akatoa wito kwa Halmashauri ya Misungwi kuongeza nguvu kwenye zoezi hilo kwani wana asilimia 27 tu.

"Ni kweli kwamba utekelezaji wa Afua za lishe hauendi vizuri kutokana na fedha kutoelekezwa kwenye eneo hilo ila nakuhakikishia Mhe Mkuu wa Mkoa kwenye bajeti mpya ya mwaka wa fedha ujao tutahakikisha shughuli zote za lishe zinakwenda vizuri." Mganga Mkuu wa Mkoa, Dktr Thomas Rutachunzibwa.

Baadae iliwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Hospitali za Halmashauri huku Ilemela wakifikia asilimia 95 hatua ya umaliziaji kwa asilimia 95 huku Misungwi wakifikia asilimia 47 pamoja na Kwimba ambao amewataka kuharakisha ujenzi bila kusahau mifumo ya TEHAMA hadi kufikia Juni 30, 2022.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti