• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mwanza aomba CAG kuja kukagua mchakato wa fedha za Mikopo kwa Makundi Maalum Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Posted on: May 30th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel ametoa agizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Ngusa Samike kumuandikia barua Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG kuja Mwanza na kuchunguza mwenendo mzima wa Vikundi vyote vilivyopatiwa Mikopo ya Makundi Maalum na Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya kubainika zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kutolewa nje ya utaratibu.


Mhe Gabriel ametoa agizo hilo baada ya kupata taarifa ya mwenendo wa utoaji wa Mikopo hiyo kutoka Kamati Maalum aliyoiunda ili kuchunguza mchakato wa utolewaji wa  fedha hizo iliyobaini Vikundi 156 ndiyo Halmashauri hiyo ina taarifa zao kati ya 337 kutoka kata 10 miongoni mwa 18 zilizopo ndani ya Wilaya hiyo.



"Nimelazimika kuitisha kikao hiki baada ya kupokea ripoti ya kamati ya kuchunguza mchakato mzima wa utolewaji wa Mikopo hii,hali siyo nzuri na nimeona ni vyema tukutane,tushauriane na kuchukua hatua lengo hizi fedha zirudi katka mzunguko"


 Mkuu wa Mkoa Mhe Gabriel ameagiza Watumishi wote wa Halmashauri hiyo wanaohusika kuratibu Mikopo hiyo wahakikishe waliowakopesha wamerejesha ili walengwa ambao ni Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu wanufaike na fedha hizo ambalo ni lengo la Serikali.


"Zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kutolewa nje ya utaratibu ni nyingi sana,hizo siyo fedha za sadaka ni lazima zirudi,haiwezekani Vikundi vingine vilivyopewa Mikopo ni vya Wanawake lakini ndani yake kuna Wanaume huu ni uchotaji wa wazi wazi wa fedha za Serikali"


Amesisitiza Vikundi vyote 680 vilivyopata Mikopo hiyo Wilayani Nyamagana vifuatiliwe na taarifa zao zijulikane baada ya ripoti kuonesha ni Vikundi 156 pekee ndiyo taarifa zake zimepatikana.


Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameruhusu kuanzia sasa mchakato wa utolewaji wa Mikopo hiyo uendelee baada ya kusimamisha kwa muda wa mwezi mmoja ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza.


Kikao hicho kimewajumuisha Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo Watumishi wa Idara za Fedha na Mipango,Kamati ya Ulinzi na Usalama, na Idara ya Maendeleo ya Jamii na Biashara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti