• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

REA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MWANZA, KILA WILAYA KUPATIWA MITUNGI YA GESI 3,255

Posted on: December 2nd, 2024

REA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MWANZA, KILA WILAYA KUPATIWA  MITUNGI YA GESI 3,255


Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) unatarajia kusambaza majiko ya gesi ya kilo sita 19,530 kwa bei ya ruzuku (Nusu bei) katika Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 02 Disemba 2024 katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, kila Wilaya itapokea mitungi 3,255 ambayo itauzwa kwa shilingi elfu 20 badala ya shilingi elfu 40, huku nusu nyingine ya gharama ikigharamiwa na serikali kupitia ruzuku.

Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi Mhandisi Mwandamizi wa Wakala wa nishati Vijijini (REA), Deusdedith Malulu amesema Serikali itagharamia shilingi bilioni 8.6 ikiwa na azma ya kufikia malengo ya Serikali ya matumizi ya 80% ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Aidha Mhandisi Malulu amesema mradi mwingine utakaogharamiwa na Serikali ni mradi wa usambazaji wa nishati ya umeme wa jua (Solar) ambapo nishati hiyo itauzwa kwa bei ya ruzuku ya 75% ambapo wanufaika ni wananchi waishio Visiwani na watapata nishati hiyo kwa shilingi laki moja hadi mbili badala ya makadirio ya shilingi laki 6.


"Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kufikisha nishati ya umeme katika maeneo yote nchini na kwa kutambua hilo imeona adha wanayoipata wananchi wa Visiwani na kuamua kuwaletea nishati ya umeme wa jua ambazo watazipata kwa punguzo la 75%".


Kadhalika mradi wa tatu ambao umetambulishwa ni mradi wa utoaji wa mikopo yenye masharti na riba nafuu iliyolenga kuwawezesha wananchi kujenga vituo vidogo vidogo vya mafuta maeneo y vijijini ili kurahisisha huduma ya upatikanaji wa mafuta maeneo ya vijijni.


"Kiasi ambacho tunatarajia kukopesha ni kuanzia shilingi milioni 133 kwa masharti nafuu kabisa na waombaji wote wanashauriwa kutembelea tovuti yetu ya www.rea.go.tz na watakutana na bango linalojieleza". Ameongeza Mhandisi Malulu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya miradi hiyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Chagu Nghoma ameishukuru REA na serikali kwa ujumla kwa kutoa ruzuku katika nishati hizo muhimu (Umeme wa Jua, majiko ya gesi pamoja na mikopo nafuu ujenzi wa Vitu vya mafuta vijijini) na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo adhimu.

"Sisi kama Mkoa tutahakikisha tunatoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya umuhimu na matumizi ya nishati safi na kuwahamasisha pia wachangamkie fursa hii ambayo Mhe. Rais amedhamiria kuwainua wananchi waishio Vijijini". Amesema Mhandisi Chagu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti