• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

REA Yatakiwa kupeleka umeme vijijini kwa wakati

Posted on: October 15th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa  mradi wa REA mkoani Mwanza kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati baada ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Akiongea kwenye  kikao cha kwanza cha bodi ya barabara ya   Mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Mhe.Mongella alisema REA limekuwa tatizo kwakuwa wananchi wa maeneo mengi hawajapata huduma licha ya REA awamu ya kwanza na ya pili kumalizika.

"REA kwa Mkoa wetu ni tatizo," alisema Mongella.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu Hilali Elisha akichangia katika kikao hicho alisema miradi ya REA haiendi vizuri wilayani Magu akibainisha ni vijiji viwili kati ya vijiji 27 ndivyo vimeanza kuunganishiwa umeme.

Akitoa ufafanuzi wa vijiji vilivyoonganishiwa umeme, Kaimu Meneja wa  Tanesco Mkoani Mwanza Mhandisi Lucas Mtabilwa alisema, Jumla ya vijiji 224 vimepata huduma ya umeme kupitia REA awamu ya kwanza na awamu pili na kufanya vijiji vyenye umeme kufikia 480 kati ya vijiji 758 vya Mkoa wa Mwanza ikiwa sawa na asilimia 63.3 ya vijiji vyote.

Mhandisi Mtabilwa alisema mradi wa REA awamu ya tatu unatarajia kugharimu Tshs.  22,999,376,085.42 na kuwa jumla ya vijiji 174 watanufaika na mradi huo.

"Awamu hii itahusisha ujenzi wa njia kubwa ya umeme yenye Urefu wa km 264.3, ujenzi wa njia ndogo yenye Urefu wa km 649, ufungaji wa transforma 319 na uunganishaji wa wateja wapya 10676," alisema Mhandisi Mtabilwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Juma Sweda aliwataka REA wajitathimini namna gani watafikia vijiji ambavyo vipo kwenye mpango kwa kuwa wananchi wanatarajia na wanahamu na umeme.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti