• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali ya awamu ya Sita kufanya mageuzi makubwa Sekta ya Elimu nchini.

Posted on: April 25th, 2023


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali ya awamu ya Sita inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo kuandaa walimu  watakaokidhi soko la ajira wanaosoma katika vyuo 35 vya ualimu  vilivyopo nchini.

Pia Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi zote za elimu kuanzia  Msingi, Sekondari, Vyuo vya kati na  Elimu ya juu ili kuleta tija kwa wahitimu wawapo katika soko la ajira.

Mhe.Prof.Mkenda amebainisha hayo leo Aprili 25,2023  jijini Mwanza wakati akizungumza na wadau wa elimu kabla hajazindua mradi wa ujenzi wa jengo la Maktaba na Maabara za Sayansi na Tehama  katika Chuo cha Ualimu nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Maelekezo ya Mhe. Rais  wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ni kwamba wanafunzi wakihitimu waweze kujiajiri  anachotaka ni elimu yetu hapa nchini  iongeze ujuzi kwa vitendo," amesema Mhe.Prof.Mkenda.

Akizungumzia miaka 59 ya Muungno wa Tanganyika na Zanzibar itakayoadhimishwa kesho April 26 2023, Prof.Mkenda amewaasa vijana wanaosoma vyuoni wasimamie muungano huo bila kuyumba, kutetereka na kubabaika ili kuwaenzi waasisi wa nchi hii.

"Chuo hiki kimeanza mwaka 1939 hadi leo vijana kutoka sehemu balimbali nchini wanakuja hapa kusoma hii ni kutokana na amani na utulivu iliyopo katika nchi yetu ambayo ni matunda ya waasisi wa nchi hii hivyo tusimame kidete kuutetea na kuulinda kwa kila hali muingano wetu,"

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amesema kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 na 2021/2022 Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk.Samia Suluhu Hassan  imeimarisha Elimu ya Ualimu kwa kupeleka fedha katika vyuo vya Ualimu kwa ajili ya mafunzo ya walimu tarajali na mafunzo kazini kwa watumishi.

 "Kupitia uimarishaji huo Chuo cha Ualimu Butimba kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 na 2021/2022 kilipokea  zaidi ya Sh bilioni moja kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara za Fizikia, Kemia Maabara ya Tehama, Vyumba vinne vya madarasa, Ukumbi wa mihadhara na kukarabati majengo ya Maabara ya Baiolojia na Maktaba.

"Pia katika kipindi cha mwaka 2021/2022 na 2022/2023 Serikali ya awamu ya sita ilileta fedha katika chuo hiki kiasi cha Sh milioni 715,163,287.28 kwa ajili ya kugharamia Mafunzo ya Ualimu kwa vitendo, mafunzo hayo hutoa fursa kwa wa wanachuo kupata tajiriba ya kumudu Maisha ya kazi na uhalisia wa Mazingira ya kazi, " amesema Mhe.Malima na kuongeza

"Pamoja na kujenga majengo ya miundombinu ya Chuo Kipya cha Murutunguru kilichopo Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2023 Serikali imepeleka fedha zaidi ya Sh milioni 369 kwa ajili ya kujenga bweni la wasichana lenye uwezo wa kuhudumia watumiaji 80 na vyumba vinne vya madarasa vyenye uwezo wa kuhudumia watumiaji 200 kwa wakati mmoja," ameeleza Mhe.Malima.

Akisoma taarifa ya mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Maabara za Sayansi, Tehama na Maktaba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof.Carolyne Nombo, Mkurugenzi Msaidizi Ualimu wa Wizira hiyo, Bwana Huruma Mageni amesema mradi huo umetekelezwa kupitia mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) kwa  gharama ya Sh Milioni 467,695,598.00.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti