• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali ya Brazil na Wadau wawapa nguvu Wakulima wa Pamba Mwanza

Posted on: July 27th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai kwa wadau wa Kilimo Mkoani Mwanza kuunga mkono jitihada zinazolenga kuboresha uzalishaji wa zao la pamba ili kuongeza kipato kwa wananchi kwani ndio zao kuu la biashara Mkoani humo.

Amesema hayo leo Julai 27, 2022 katika kikao kilichofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mjini humo cha Kamati ya Uendeshaji Mradi wa zaidi ya Pamba 'Beyond Cotton' wenye thamani ya zaidi ya Tshs Bilioni 2 chini ya udhadhili wa Serikali ya Brazil na wadau wengine.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amefafanua kuwa Miongoni mwa manufaa ya zao la Pamba ni kuwa linavumilia ukame ukilinganisha na mazao mengine hasa kwa kuzingatia mabadiriko ya tabia nchi ambapo mkoani humo wamekua wakikumbwa zaidi ya mabadiriko hayo.


Vilevile, Mkuu wa Mkoa ameishukuru Serikali ya Brazil kupitia 'Brazilian Cooperating Agency' kwa ufadhili wa Mradi huo nchini na ametoa rai kwa watumishi wa wizara ya Kilimo kuongeza ushirikiano kwenye mradi huo ambao utasaidia sana kufikia adhma ya serikali ya awamu ya sita ya kuinua kilimo ambacho ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi.

Amefafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwainua wananchi wapatao takribani asilimia 65 waliojiajiri kwenye Kilimo na ndio maana imegawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani ambapo kwa Mwanza pekee wamepata Pikipiki 45 huku ikidhamiria kuwapatia maafisa Ugani wote 274 waliopo Mkoani humo.


Aidha, ametoa wito kwa wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu wa Kilimo juu ya taratibu za kufuatwa kwenye kilimo cha pamba ili waweze kupata mazao mengi kama suala la upandaji wa kufuata sentimita 30 kwa 60 kati ya mche kwa mche na mstari kwa mstari ambayo husaidia kuongeza mazao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti