• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Somo la Michezo lifundishwe Shuleni ,Vyuoni – Majaliwa

Posted on: June 9th, 2018

Somo la  Michezo lifundishwe Shuleni ,Vyuoni – Majaliwa

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema kuwa somo la elimu ya Michezo linatakiwa kufundishwa kuanzia shule za msingi,sekondari hadi vyuo vikuu ili kukuza viwango vya michezo na vipaji kwa vijana Tanzania.


Mhe. Majaliwa alisema hayo  Mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, wakati akifungua rasmi mashindano ya shule za Sekondari na  msingi( UMISSETA na UMITASHUMTA) Taifa kutoka Mikoa 26 ya Tanzania bara na Mikoa 2 kutoka Unguja na Pemba Zanzibar.


“Kauli mbiu yetu mwaka huu katika  Mashindano ya umiseta na umishumitani,Michezo, Sanaa na Taaluma ni Msingi wa maendeleo ya wanafunzi katika Taifa letu,”alisema Majaliwa.


Mhe. Majaliwa aliongeza  kuwa Serikali imeweka kipaumbele katika suala la  michezo mashuleni,huku akizitaka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,  kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha somo la michezo linafundishwa kuanzia shule za msingi, Sekondari hadi vyuo vikuu ikiwa lengo ni kukuza kiwango cha michezo Nchini na vipaji kwa vijana.


Aliziagiza Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinatenga bajeti kwa  ajili ya michezo katika shule za msingi na Sekondari na kuwapa fursa walimu wenye uwezo wa kufundisha michezo shuleni ,badala ya kuwapa bora walimu kufundisha somo hilo.


Waziri Majaliwa amewaonya maofisa Elimu na walimu wa michezo mikoani kutohujumu mashindano hayo kwa kuingiza watu wasio wanafunzi kushiriki ambao ni ’’ Mamluki”kuwa wakigundulika wamefanya hivyo hatua kali dhidi  yao zitachukuliwa na Serikali.

Awali naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Leonard Akwilapo amesema kuwa mashindano hayo yamelenga kuibua wanamichezo nchini kutengeneza ajira ambapo tayari baadhi ya vijana wamefanikiwa kutokana na michezo.


Mhe. Akwilapo amesema mfano wa  wachezaji wa mpira wa miguu ambao wamefikia kiwango bora waliotokana na michezo shuleni ambao ni Edibily Lunyamila aliyewahi kuchezea timu ya Yanga, Shiza Kichuya ambaye ni mchezaji nyota wa Simba na Mbwana Samatta ambaye kwa sasa yuko nchini Ubeligiji akichezea timu Genk iliyopo ya ligi kuu .

Naye Mwalikishi wa kampuni ya COCA COLA ambao ni wadhamini wa mashindano hayo ,David Kalamagi wameahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo na kufanya maboresho kwenye baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza wakati wa  mashindano hayo.


Mashindano hayo ya Umiseta na Umitashumita yameshirikisha jumla ya wanafunzi 6480 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti