• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TANESCO SACCOS Yatoa msaada wa mashuka Hospitali Nchi nzima

Posted on: May 20th, 2018

Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo TANESCO (TANESCO  SACCOS LTD),Tawi la Mkoa wa Mwanza kimetoa msaada wa mashuka 140 kwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure Mkoa wa Mwanza.

Akikabidhi mashuka hayo Meneja wa TANESCO SACCOS  LTD Taifa Andre Hilary amesema iko haja ya wadau wengine kuthamini watu wenye mahitaji maalumu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanesco kiliandikishwa mwaka 1843 na kupata namba ya usajili mwaka 1968  ambapo Uanachama ndani ya TANESCO SACCOS uko wazi kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme – TANESCO, Wafanyakazi wa TANESCO SACCOS, Wastaafu wa TANESCO, Wafanyakazi wa muda Maalum wa TANESCO, Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na  Kampuni au Taasisi zilizo katika sekta ya Nishati.

“Chama hiki kilianzishwa kikiwa na lengo la kuhamasisha wanachama wake kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kuwapa fursa ya kukopa kwa riba nafuu kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi,”alisema Hilary.

 

TANESCO SACCOS kupitia mpango Mkakati wa miaka mitano 2014-2018 unatekeleza msingi namba 7  wa Ushirika wa kuijali jamii (Concern for the Community). Katika Mpango huo Chama kinatoa msaada  katika sekta ya Afya kwa kutoa Mashuka katika Hospitali za Rufaa za Mkoa Nchi nzima.

 Zoezi hili ni zoezi endelevu lilionza mwaka 2014 kwa taasisi ya magonjwa ya kansa ya Ocean Road  na kuendelea na Hospitali zote nchini.

Mikoa iliyopatiwa msaada kwa mwaka huu ni pamoja na Mwananyamala RRH Dar es Salaam, Songea RRH Ruvuma,Amana RRH,Temeke RRH in Dar es Salaam,Dodoma RRH, Ligula RRH Mtwara, Mbeya Zonal RH, Mount Meru RRH Arusha, Morogoro RRH,hizi Hospitali zote zilipata mashuka 150 kila moja.

 Hospitali ya Kitete RRH Tabora na Geita RRH ambao walipata mashuka 130 kila Hospitali wakati Hospitali ya Sekou Toure RRH imepata mashuka 140 na kukamilisha jumla ya mashuka 1750 yaliyotolewa hadi sasa.

Aidha, Dira ya TANESCO SACCOS ni kuwa SACCOS inayoongoza Nchini Tanzania  inayokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya wanachama wake kupitia huduma bora za kifedha ikiwa na Dhamira ya kuhamasisha na kuimarisha ukusanyaji wa akiba, hisa na amana kupitia utoaji wa elimu ya mikopo na huduma bora kwa wateja.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti