• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TATHMINI NI KIOO – RC MTANDA

Posted on: July 2nd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kufanya tathmini ni muhimu, inakufanya uone na kutambua nguvu na udhaifu hivyo ameifananisha kama kioo ambapo amesema kinatoa fursa ya kujitazama.


Mkuu wa Mkoa amesema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao cha Watumishi wa Sekta ya Ardhi Mkoa wa Mwanza leo julai 02, 2025 na kuipongeza sekta hiyo kwa wazo hilo kwani watapata fursa ya kutambua na kurekebisha mahali walipokosea ili waweze kufikia malengo.

“Mtu yoyote anayependa maendeleo lazima ajifanyie tathmini ya mwaka mzima, ni watu wachache wanaopenda kufanya tathmini, unapojitathmini utajua wapi pa kurekebisha”.


Aidha, Mhe. Mtanda amekitaka kikao hicho kutokujikita katika sekta ya ardhi pekee bali pia kuwafanyia tathmini wale aliowaita wasukumaji wa sekta hiyo ( Wataalamu wa Ardhi).

“Mnaweza kukaa humu ndani mkajifungia mkaongea na mpaka muda wa chakula ukafika mkala lakini kumbe mnafanya tathmini ya uongo, sasa ni lazima muambiane ukweli” Amesema Mkuu wa Mkoa


Kadhalika Mkuu wa Mkoa amewataka Wataalamu wa Ardhi kushughulikia migogoro ya ardhi kwa kudhibiti kutokuibuka kwa migogoro mipya na kushughulikia migogoro iliyopo kwa weledi.

Kuhusu ukusanyaji wa maduhuli, Mkuu wa Mkoa ameitaka sekta hiyo kuhakikisha wanaongeza hamasa na ufuatiliaji katika ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha elimu ya ulipaji kodi ya ardhi inatolewa mara kwa mara ili kuwepo na ushirikishwaji wa wananchi.


Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kunakuwepo na operesheni za Wilaya kwa Wilaya kuhusu kliniki za ardhi walau mara mbili kwa mwaka.


Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza Bw. Wilson Lugi amesema wamekutana kama wataalam kufanya tathmini ya kiutendaji ya mwaka 2024/2025 na kupanga namna ya kufanya vyema 2025/26.

Kamishna huyo wa Ardhi Msaidizi amesema wametekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa hati, usimamizi na utekelezaji wa miradi mbalimbali, Pia wamefanikiwa kukusanya maduhuli ya Serikali zaidi ya sh. Bilioni 8.7 sawa na 42% ya makusudio.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti