• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TCRA Yatoa elimu kwa Wadau wa Huduma za Mawasiliano

Posted on: April 4th, 2019

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  imefanya Mkutano na wadau  wa huduma za mawasiliano  Mkoa wa Mwanza  ikiwa na lengo la kukumbushana taswira ya Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya mwaka 2015,Matumizi bora ya mitandao ya kijamii,changamoto za watumiaji wa mawasiliano na kuelimisha Umma na utatuzi wa malalamiko hayo.

Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Kanda ya Ziwa Mamlaka ya Mawasiliano Mhandisi Fransis Mihayo amesema kutokana na ukuaji wa tekinolojia kumekuwa na uelewa mdogo wa watumiaji wa mitandao hivyo kifanya makosa ya kimitandao kuongezeka kila siku.

" Mamlaka inayo orodha ya watoa huduma mitandaoni wanaoendelea kurusha maudhui kwa kuvizia, inawataadharisha kuacha kuvunja sheria, bali wafuate taratibu za usajili,"alisema Mhandisi Mihayo.

Aidha amewaomba viongozi wa dini wakati wakiendelea kutujenga na kutuimarisha kiroho, watukumbushe pia uwepo wa changamoto ya matapeli mitandaoni na kamwe kila mtu hapaswi kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa kujibu ujumbe mfupi na kuendelea na mazungumzo na matapeli kupitia simu.

Naye Kamishna Msaidizi wa polisi Muliro J.MULIRO amesema maendeleo makubwa  ya kitekinolojia yameleta ongezeko kubwa la huduma mbalimbali mitandaoni, na kuleta msukumo mkubwa wa ukuaji katika Sekta ya mawasiliano.

"Mwaka 2000 kulikuwa na laini za simu 284,109 idadi hii imeongezeka hadi laini milioni 43 kwa sasa wakati huduma za intaneti wameongezeka  kutoka milioni 3 na laki tano kwa miaka 5 iliyopita hadi milioni 17 hivi leo," alisema Kamishna Muliro.

Kwa upande wao watoa huduma kutoka Vodacom wakiwakilishwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa Victoria, Ayubu Kalutya  amesema wao hufanya kazi hadi jumamoai hivyo wangependa hata Jeshi la polisi lingefanya hivyo hasa wanaohuaika na taarifa ya upotevu 'loss report' kwani wateja huchukua muda mrefu kupata taarifa hii, pia huwachelewesha kurudisha line zao.

"Kuwe na udhibiti wa simu ili makampuni yanayotoa huduma za simu yaweze kuendesha huduma kuwezs kuwa na mawasiliano mazuri na wateja wao,"alisema Kalutya.

Aidha Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha uhalifu wa kimtandao kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, ASP Joshua Mwangasa amesema, kuna changamoto kubwa ya kutoa taarifa za uongo hivyo jeshi la polisi linakabiliana na kila mvunjifu wa kosa hilo, hata hivyo ushirikiano mkubwa kati ya Jeshi la polisi na wananchi inasaidia kuleta amani.

"Ili kuepuka kufanya makosa ya mtandao  ni vema kufuata sheria,kuwa na hofu ya mungu, kuepuka kutuma taarifa udiyo na uhakika nayo na kuhakikisha kila mtu anatoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ualifu unapotokea,"alisema ASP Mwangasa.

Aidha, ushirikiano unatakiwa ili kuleta amani kwani baadhi ya mitandao ya kijamii ipo nje ya nchi hivyo Mamlaka ya Mawasiliano haina mamlaka nayo.

Hata hivyo amesisitiza kuwa uvunjifu wote wa sheria uripotiwe polisi ili wahalifu wakabiliwe na sheria ifuate mkondo wake, pia ulinzi uanzie kwa mtu mwenyewe.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti