• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TUENDELEE KUSHIKAMANA WANA MWANZA PAMBA JIJI FC ITIMIZE LENGO LA KUCHEZA LIGI KUU MSIMU UJAO-RC MAKALLA

Posted on: September 15th, 2023

TUENDELEE KUSHIKAMANA WANA MWANZA PAMBA JIJI FC ITIMIZE LENGO LA KUCHEZA LIGI KUU MSIMU UJAO-RC MAKALLA


*Asema siri ya kufikia malengo ni mshikamano wa pamoja kutoka kwa mashabiki


*Aonesha matumaini ya kucheza Ligi kuu kutokana na ubora wa Pamba Jiji FC


Wakati wana TP Lindanda wakiendelea kung'ara kwa mfululizo wa ushindi michuano ya soka  Ligi ya Championship kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pan African,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makalla ameendelea kuwaomba mashabiki wa soka kuendelea kuipa ari timu hiyo kwa kufurika uwanjani katika kila michezo ya timu hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye pia ni mlezi wa timu biyo akizungumza na vyombo vya habari leo kwenye uwanja wa Nyamagana mara baada ya mpambano,amesema huu ni mwanzo mzuri ambao unaleta matumaini ya kucheza Ligi kuu msimu ujao.

"Siku zote shabiki uwanjani ni mchezaji wa 12  hivyo napenda kuwaomba tuendelee kushikamana kwa pamoja kwa lengo la kuwatia moyo wachezaji wetu wazidi kufanya vizuri,"Mhe.Makalla

Mhe.Makalla amebainisha Ligi ya Championship ni ngumu kutokana na timu zinazopambana kupanda Ligi kuu ni nyingi na zenye uwezo,hivyo wajibu wa kila mwana Mwanza ni kuwaunga mkono wana TP Lindanda.

Katika mchezo huo Pamba Jiji FC walilazimika kupata ushindi huo muda wa lala salama kwa mkwaju wa penati uliofungwa na mchezaji Jamal Mtegeta na kuamsha shamra shamra na nderemo kutoka kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

Mara baada ya filimbi ya mwisho kuashiria kuhitimisha mpambano huo,mlezi wa timu hiyo akiongozona na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe.Amina Makilagi,Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Mhe.Stanslaus Mabula na Meya wa Jiji Mhe.Sima Costantine Sima walishuka uwanjani na kuwapongeza Pamba Jiji FC kwa ushindi huo.

Wana TP Lindanda msimu huu wakiwa na mchanganyiko mzuri wa wachezaji waliotamba Ligi kuu msimu uliopita,mchezo wa fungua dimba uliopigwa uwanja wa Nyamagana waliichakaza timu ya Cosmo Politan kutoka Da- re-Salaam kwa mabao 4-0 kabla ya leo kuwafunga Pan African bao 1-0

Baada ya michezo hiyo miwili ya nyumbani ya Ligi ya Championship,Pamba Jiji FC sasa mchezo ujao watasafiri hadi Shinyanga kuumana na Stendi Utd Ijumaa ijayo kwenye dimba la Kambarage.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti