• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

UJENZI DARAJA LA KIGONGO-BUSISI WAFIKIA 88.2%, RC MTANDA ASEMA HAKUNA KILICHOSIMAMA

Posted on: June 10th, 2024

UJENZI DARAJA LA KIGONGO-BUSISI WAFIKIA 88.2%, RC MTANDA ASEMA HAKUNA KILICHOSIMAMA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa daraja la JPM (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa KM 3.2 linalojengwa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya zaidi ya Tshs. Bilioni 716.

Mtanda amesema chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, ujenzi wa daraja hilo  umefikia asilimia 88.2 na akatumia wasaa huo kuwapongeza kwa kazi nzuri na akatoa wito kuendelea kusimamia ili ukamilike kwa wakati ifikapo Disemba 30 mwaka huu.

Mtanda ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kujenga daraja hilo kwa kasi kwani Rais Samia amelikuta likiwa chini ya asilimia 40 kiujenzi na hata malipo ya fedha lakini ndani ya miaka mitatu limeendelezwa bila kusimama na kwamba sasa wananchi wataondolewa adha ya msongamano kwenye vivuko.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutatoa fursa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa na nchi za jirani kuwa na hakika wa kufika kwa urahisi vilevile utasaidia kupunguza msongamano w magari kwenye vivuko vinavyotumika sasa na kwamba utarahisisha suala la usafiri kwa ujumla.

Mwakilishi wa Meneja wa TANROAD Mkoa huo Mhandisi Richard Ruyango amesema awali ujenzi wa daraja hilo  ulioanza mwaka 2020 ulitarajiwa kukamilika Februari mwaka huu lakini kutokana na sababu mbalimbali mkandarasi huyo aliongezewa muda.

"Hatujaona mpango wa kujenga mzani upande wa Sengerema hivyo tunaomba ujengwe ili kulinda daraja letu maana uwekezaji huu ni lazima ulindwe kwa kuweka ukomo wa uzito wa magari kupita ili lidumu muda mrefu." Mhe. Hamis Tabasam, Mbunge wa Sengerema.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti