• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Ukerewe Yawezeshwa Vifaa Tiba

Posted on: April 8th, 2019


Hospitali ya Uhuru  imetoa msaada wa hadubini mbili ‘microscope’ zenye thamani ya  Sh milioni 6 kwa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya vifaa tiba hasa za uchunguzi.

Akikabidhi  mashine hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Uhuru, Dkt. Derrick Nyasebwa, Mkurugenzi wa Tiba na bingwa wa upasuaji, Dkt. Emmanuel  Kanumba alisema  kama taasisi imefikia hatua ya kuisaidia Wilaya ya Ukerewe kutokana na ombi lao.

Dkt. Kanumba alisema  mazingira ya wilaya ya Ukerewe  yalivyo inapaswa kusaidiwa katika sekta ya afya kwani  bila wananchi wa kisiwa hicho kuwa na afya njema hakuna maendeleo yatakayopatikana.

“Taasisi ya Uhuru hosptali  inashirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha suala la afya halibaki kuwa jukumu la watu fulani bali ni   la wote hivyo  tumetoa msaada wa microscope  baada ya kubaini upungufu huo uliopo katika wilaya ya Ukerewe.

Mara zote tumekuwa tukishiriki katika vikao mbalimbali vya sekta ya afya lakini  taarifa nyingi kutoka Ukerewe ni upungufu wa vitendea kazi, sasa tukaona ni heri tukasaidia hizi mashine na imani yetu masuala ya vipimo vya maradhi  hayatakuwa na shida tena,”alisema Dkt. Kanumba.

Dkt. Kanumba alisema hivi karibuni Serikali imezindua kampeni ya  uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi iliyokuwa na kauli mbiu ya ‘Jiongeze Tuwavushe salama’ hivyo  kama taasisi ya  Uhuru imeshiriki vema kwa kutoa mashine hizo ambazo zitakwenda kupima maradhi ya wagonjwa watakaofika  hospitalini kupata tiba.

Alisema wamekuwa na utaratibu wa kusaidi jamii pale inapohitajika ambapo aliongeza kwamba hata watoto yatima hutibiwa bure na wale wenye kipato duni hutibiwa kwa gharama nafuu.

Aliwataka jamii kutoogopa kwenda hospitali za binafsi kwani kwa kuogopa gharama bali huwa zinasikiliza  maombi ya mgonjwa na kumtibu kwa gharama nafuu.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Lucas Magembe, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, alishukuru uongozi wa hospitali hiyo kuona umuhimu wa kuisaidia jamii.


Kipole alisema vifaa hivyo vitakwenda kuitumiaka kama ilivyokusudia  na kuwataka watumishi ndani ya wilaya hiyo kuituna mashine hiyo ili iweze kuwasaidia wananchi wengi.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella aliwasainisha  kiapo  cha uwajibikaji wakuu wa wilaya zote za mkoa huo  juu ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga ambapo aliwataka kila mmoja awajibike katika eneo lake na  kutoa taarifa ya utekelezaji kila baada ya miezi mitatu.

Tukio hilo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi iliyokuwa na kauli mbiu ya ‘Jiongeze Tuwavushe salama’   ambapo Mhe.Mongella alisema takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2017 jumla ya wanawake 195 walipoteza maisha kutokana na uzazi huo.

Mongella alisema kutokana na jitihada za Serikali za kupunguza haali hiyo, mwaka 2018 vifo hivyo vimepungua na kufikia 151 lakini kuanzia Januari mwaka huu tayari vifo 46  vitokanavyo na uzazi vimetokea ndani ya mkoa huo.






Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti