• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Upimaji wa Virusi vya UKIMWI waongezeka Mwanza

Posted on: December 1st, 2018

Upimaji wa Virusi vya UKIMWI waongezeka Mkoani Mwanza.Hayo yamebainishwa leo katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo yamefanyika Kimkoa katika Viwanja vya Furahisha wilaya ya Ilemela.

Akiongea kwenye Maadhimisho hayo Mgeni rasmi Mhe. Dkt Severin Lalika amesema Upimaji wa VVU umeongezeka Zaidi katika Mkoa wetu kupitia kampeni iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza tarehe 21/07/2018 katika viwanja vya furahisha ambapo kwa siku hiyo peke yake watu 2006 walipimwa wanaume wakiwa 1,234 na wanawake wakiwa 772 na jumla ya watu 167 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU,wanaume 94 na wanawake 73

Aidha Halmashauri ziliendelea na Kampeni hiyo ya upimaji na kufanya jumla ya watu 714,842 kupima afya zao ,wanaume 252,539 na wanawake 462,303 ambapo kwa Idadi hiyo watu 8,197 waligundulika kuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI

Mhe.Dkt Severin amesema kutokana na Takwimu zilizopo zinazoonesha Maambukizi ya UKIMWI Mkoani Mwanza zimepanda kutoka Asilimia 4.2 mpaka Asilimia 7.2 kwa Mwaka 2016/17  hivyo kuwataka wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono Jitihada zinazofanywa na wananchi pamoja na wadau mbali mbali za kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI

Akitoa Salamu za Nyamagana Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt.Phillis Nyimbi amesema kutokana na takwimu za maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,Nyamagana imeonekana inaongoza kuwa na Idadi Kubwa ya maambukizi  ambapo watu 23,583 wamegundulika kuwa na Virusi vya UKIMWI“Mimi kama msimazi mkuu wa wilaya ninalichukua hili na kwenda kuwashirikisha viongozi wengine wilayani kwangu na kulifanyia kazi”  amesema Dkt Nyimbi

Aidha Dkt Nyimbi amewataka wadau mbali mbali wanaojishughulisha na shughuli za Afya kufika Ofisini kwake nayeye yupo tayari kutoa ushirikiano kupunguza kiwango hicho cha maambukizi

Akisoma Taarifa ya Maambukizi ya UKIMWI kimkoa Mratibu wa UKIMWI Mkoa Dkt Pius Masele amesema kwa Takwimu za Mwaka 2017 /18, Mwanza umekua Mkoa wa Nne kitaifa kuwa na Idadi kubwa ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ambapo kiwilaya Nyamagana ikishika nafasi ya Kwanza kuwa na Idadi ya watu 23,583 walioambukizwa VVU



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti