• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Vijana 194 wahitimu Mafunzo ya Atamizi Mwanza,wapewa Rai ya kutanua wigo wa kujiajiri

Posted on: May 29th, 2023

*Vijana 194 wahitimu Mafunzo ya Atamizi Mwanza,watakiwa kutanua wigo wa kujiajiri


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewapongeza na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo ya Atamizi kuziendeleza juhudi za serikali za kuongeza fursa ya ajira kwa vijana kwa kujiajiri na kuwaajiri wengine.

Mhe. Ulega ameyasema hayo leo Mei 29 wakati alipohudhuria hafla ya ufungaji mafunzo hayo ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji yaliyo chukua muda wa Miezi 3 ambayo imewakusanyisha wahitimu 194 wa awamu ya kwanza kutoka katika vituo 14 nchi nzima iliyofanyika Mkoani Mwanza katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Butimba.

"Nipende kuwapongeza vijana mnaohitimu  leo kwa hatua mliochukua ya kujifunza uvuvi kwa nia ya kuanzisha miradi ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji inachangia kwa kiasi kikubwa kukuza juhudi za serikali za kukuza fursa za ajira  kwa vijana kupitia sekta ya uvuvi,"Amesema Mhe. Ulega.

"Kwa mwaka 2023/2024 wizara imepanga kuwawezesha vijana 750 kupata mafunzo kwa vitendo kwa vijana waliohitimu katika fani ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe  maji nchini miongoni mwao watakua ni vijana waliopo katika mafunzo ya JKT."  Mhe. Ulega.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Amos Makalla amesema sekta ya uvuvi inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza uchumi wa Mkoa wa Mwanza.

"Sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa katika kuinua uchumi kwenye Mkoa wa Mwanza shughuli ya uvuvi ni sehemu ya ajira kwa wananchi walio wengi kupitia biashara za samaki, kutengeneza vyombo vya kuvulia samaki na kwenye viwanda vya kuchakata Minofu ya samaki  hadi kufikia  Machi 2023  ambayo ni robo tatu ya mwaka wa fedha  2022/2023 zaidi ya Shilingi Bilioni moja zilikusanywa kutoka sekta ya uvuvi  zikiwa ni sawa na 31.125% ya makusanyo ya Mkoa",amesema Elikana.

Aidha, Bi. Happiness Meena, Naibu Katibu Mkuu Wizara  Mifugo na Uvuvi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea Vijana ujuzi kwa vitendo zaidi  ili waweze kuongeza ubunifu katika kile ambacho wamejifunza.

Vilevile, mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi Vijana Ajira na wenye ulemavu Bi. Josephine Mwaijande amesema Ofisi yao ipo katika taratibu za  kujenga kituo kimoja cha kutoa mafunzo hayo katika mwali wa Katongo Mkoani Kigoma

Pia, Bi. Jovina Eliam ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo kutoka Dar es salaam  wakati akisoma Risala ameiomba serikali kuwapatia vitambulisho ambavyo vitawatambulisha kama wataalam na wabobezi wa maswala ya uvuvi na kuwatofautisha na wale ambao watakua hawajabobea katika mafunzo hayo

Lengo la mafunzo hayo ya ATAMIZI ambayo yamechukua ni kuwajenga vijana walio hitimu fani ya uvuvi  na ukuzaji wa viumbe maji ni kuondoa dhana ya kuajiriwa na hivyo kuweza kubuni miradi na kuanzisha kampuni hivyo kuchangia katika pato la Taifa na kutoa fursa za ajira kwa watanzania.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti