• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Viongozi wa Umma waaswa kujiepusha na migongano ya maslahi

Posted on: May 5th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima ameziagiza halmashauri zote zilizopo mkoani humo kutoa mafunzo kwa Viongozi wa umma ili kuwakumbusha kutenda kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, maadili na uadilifu wa utumishi wa umma.

Mhe. Malima amesema kumekuwa na mmomonyoka mkubwa wa ukiukwaji maadili kwa baadhi ya  watumishi wa umma   wanapotekeleza majukumu yao ikiwemo miradi ya maendeleo hali inayosababisha itekelezwe chini ya kiwango ikiwa haina thamani halisi ya fedha.

 Mhe. Malima ameyasema hayo leo Mei 5, 2023 wakati akifungua mafunzo ya maadili kwa viongozi wa umma wa Mkoa wa Mwanza yaliyolenga kuwakumbusha viongozi na wakuuu wa taasisi za umma mkoani humo kuzingatia kanuni, sheria na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao, kujiepusha na masuala yote yanayoweza kuwaingiza kwenye mgongano wa maslahi na kuzingatia suala la uwajibikaji wa pamoja.

“Maadili ni nguzo muhimu sana katika kufanikisha mipango ya maendeleo, viongozi wa umma zingatieni hilo hasa zile Taasisi zinazotekeleza miradi  mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi  kwa mfano MWAUWASA, TARURA, RUWASA, TANESCO na REA mnapokosa uadilifu mkakoroga mradi anayetukanwa na wananchi ni Mhe. Rais na Chama cha Mapinduzi wakati lengo la Serikali ni kuinua maisha ya wananchi kiuchumi ndani ya mkoa wa Mwanza sitawavumilia”amesema Mhe. Malima.

Naye, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa, Godson Kweka, amesema mafunzo hayo yana mada tatu ambazo ni Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo wanakumbushana misingi ya Maadili ya Umma kama ilivyoainishwa kwenye Sheria hiyo, mgongano wa maslahi na Uwajibikaji wa pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tunawakumbusha Viongozi wa Umma Mkoa wa Mwanza kuishi na kuheshimu viapo vyao vya ahadi ya uadilifu walivyoapa kwa nyakati tofauti walipopewa dhamana ya nafasi walizonazo kwa sasa kipaumbele kikubwa cha  sekretarieti ya maadili ya umma pamoja na mambo mengine ni kuhimiza suala zima la uwajibikaji wa pamoja kwa viongozi, watumishi na wananchi katika ushirikishwaji ili kuwaletea wananchi maendeleo,”amsesema na kuongeza.

“Sisi sote ni mashahidi, hatuna shaka na tunakila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyotafuta fedha za kutekeleza miradi mbalimbali  katika halmashauri zetu  kwa ajili ya  kuwaletea wananchi maendeleo  miradi hiyo inahitaji kuwa na viongozi waadilifu kwenye usimamizi wa fedha na usimamizi wa rasilimali zingine ambazo zipo kwenye maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana, amewataka watumishi wa umma  kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa wazalendo ili kukidhi matarajio ya wananchi kwa serikali yao katika kuwaletea maendeleo.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti