• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wadau wa Sekta ya Maziwa punguzeni bei ili mpango wa kunywa Maziwa shuleni ufanukiwe : Naibu Waziri Mnyeti

Posted on: September 27th, 2023

Wadau wa Sekta ya Maziwa punguzeni bei ili mpango wa kunywa Maziwa shuleni ufanukiwe : Naibu Waziri Mnyeti


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewaomba wadau wa tasnia ya maziwa nchini kupunguza bei ya maziwa ya Shs 1800 kwa nusu lita ili mpango wa kunywa maziwa watoto wote shuleni ufike malengo.

Kauli hiyo imetolewa leo kwenye viwanja vya Furahisha Mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya unywaji maziwa shuleni Duniani ambapo Kitaifa imefanyika Mkoani humo.

Mhe. Mnyeti amesema Serikali imefuta tozo zote zinazohusu maziwa hivyo  mamlaka husika ziangalie bei muafaka eneo la vifungashio ili wadau wa tasnia hiyo wasiingie gharama kubwa.

"Bado Mkoa kama wa Mwanza unakabiliwa na hali ya udumavu wa watoto hii imechangiwa na ukosefu wa lishe bora, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha unywaji wa maziwa uwe sehemu ya mlo wa mtoto shuleni." amesisitiza Mhe.Mnyeti.

Amesema itakuwa ni kazi bure kuendelea kuhimiza unywaji wa maziwa kila Ifikapo kilele cha maadhimisho hayo wakati uwezo wa kumudu hali hiyo haupo kutoka kwa wazazi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi ameishukuru Wizara kwa kuona umuhimu wa maadhimisho hayo kufanyika Mkoani humo kutokana na miradi mingi ya kuboresha mifugo inatekelezwa kuanzia Shamba la Taifa la Mifugo Mabuki na kwenye baadhi ya wilaya.

"Mhe. mgeni rasmi Serikali ya awamu ya sita imeleta mitamba 500 Mkoani Mwanza kwa ajili ya kuleta tija ya maziwa na nyama kwa wafugaji, pia wapo vijana wanaopatiwa mafunzo maalum ya ufugaji wa kisasa huko Mabuki," Mhe.Makilagi.

"Bado tuna changamoto ya unywaji wa maziwa nchini ambapo hadi sasa mtu mmoja anakunywa lita 62 kwa mwaka wakati kwa mujibu wa mwongozo wa kimataifa mtu mmoja anatakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka, hivyo inahitajika kazi ya ziada kuhamasisha jamii umuhimu wa kunywa maziwa," Dkt.George Msalia,Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini TDB.

Kuelekea kilele hicho Bodi ya Maziwa ilifanya zoezi la ugawaji wa maziwa shuleni na utoaji wa elimu kwa baadhi ya shule Mkoani Mwanza pamoja na kufanya kongamano lililowahusisha wadau wa tasnia ya maziwa na walimu.

Kila  Jumatano ya mwisho wa Septemba Tanzania inajumuika na Mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya unywaji maziwa shuleni ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Mpe mtoto maziwa kwa maendeleo bora Shuleni"

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti