• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

"Wafanyabiashara waliopisha ujenzi wa Stendi kuu ya Nyegezi wapewe kipaumbele" Mhe Majaliwa

Posted on: October 18th, 2022


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameutaka uongozi  wa Halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha wafanyabiashara wote waliokuwa wanafanya biashara Stendi Kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani ilipojengwa mpya katika Kata ya Nyegezi wapewe  kipaumbele kupata maeneo ya kufanyia biashara.

Mhe.Majaliwa ametoa agizo hilo  Oktoba 17,2022 wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo  inayojengwa  kwa fedha za serikali Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kwa gharama ya Sh bilioni 15,885,589,063 na mkandarasi Mohammedi Builders Ltd.

"Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati lengo ni kuwanufaisha wananchi wake na mmeniambia kwamba mmejenga stendi hii nzuri kabisa ya  kifahari  lakini kuna eneo limebaki hivyo endapo maeneo yaliyopo ndani ya stendi hii yatakuwa machache kuwatosha wafanyabiashara wote  waliokuwa wakifanya biashara zao hapa awali wajengeeni kwenye eneo hilo.

" Maana Rais Samia Suluhu Hassan ameleta Shilingi bilioni tisa katika jiji la Mwanza kwa ajili ya kujenga masoko  nia na dhimira yake ni kuwaandalia na kuwajengea  machinga maeneo yao ili wafanye biashara zao katika mazingira  bora, amesema na  nyie wafanyabiashara mliokuwa mnafanya biashara kwenye stendi hii zamani kabla ya ujenzi wa hii mpya haujaanza kama kwa sasa hautafanya tena biashara  toa taarifa kwenye uongozi wa jiji ili wengine wanaohitaji wagawiwe maeneo usikae kimya,"ameagiza Mhe. Majaliwa.

Aidha, amewataka wananchi wa Mkoa wa Mwanza wajipange kwa ajili ya

kunufaika na miradi mikubwa ya kimkakati inayojengwa mkoani humo ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR), daraja la kigongo busisi maarufu kama Daraja la J.P Magufuli, stendi hiyo ya Nyegezi na iliyojengwa Wilaya ya Ilemela ambapo amewahakikishia wananchi kwamba hakuna mradi wowote wa kimkakati unaotekelezwa ndani ya mkoa huo  utakaokwama  maana fedha zipo na tayari serikali imeishazitenga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Yahya Sekiete amesema hadi sasa  mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 98 ingawa ulikumbwa  na changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama saruji, nondo kutokana na kupanda kwa bei, bati za geji 26 zilizokuwa hazipatikani nchini pamoja na baadhi ya vifaa vinavyoagizwa nje ya nchi kuchelewa kufika bandarini.


" Mradi huu ulianza kutekelezwa Februari 5, 2019 ukikamilika utasaidia kuongeza mapato ya halmashauri ya jiji la Mwanza hivyo kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu pia utalifanya jiji la Mwanza kuwa la kisasa zaidi, utasaidia kukua kwa biashara nyingine kutoka mikoa mbaimbali  na nchi jirani.

Ametaja maeneo yatakayokuwepo baada ya mradi huo kukamilika kuwa ni pamoja na  eneo la maegesho ya mabasi 120, madogo 80 kwa wakati mmoja, maduka makubwa 14, madogo 60, sehemu tatu za abiria  wapatao 7400 kusubiria mabasi, vyoo saba vyenye matundu 63 jengo la abiria, benki, vibanda 38 vya kukatia tiketi na vibanda vya mama lishe na eneo maalum kwa ajili ya wanawake wanaonyonesha.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti