• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wakulima waaswa kujiunga vyama vya ushirika

Posted on: September 28th, 2019

Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe amewatahadharisha wale waliohusika na upotevu wa fedha shilling billion 123 za wakulima kupitia kwenye vyama vya ushirika vya kilimo na masoko ( AMCOS) watachukuliwa hatua za kisheria ili kuurudisha ushirika huo katika mstari na kuhakikisha haki ya mkulima inalindwa.
 
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe wakati wa mkutano wa 16 wa wadau wa sekta ndogo ya  pamba Tanzania uliowakutanisha wakulima, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakurugenzi, wabunge na viongozi vyama vya ushirika kutoka mikoa 17 ya Tanzania bara inayolima zao la pamba ,  uliofanyika jijini hapa lengo likiwa kuongeza tija katika zao hilo hivyo alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale waliohusika na upotevu wa fedha hizo.

" Hili hatutalifumbia macho kwa sababu  hakuna watu wanaowaibia wakulima kama vyama vya ushirika vya kilimo na masoko (AMCOS ) kwa mujibu wa wakaguzi wa mahesabu ya ndani (COASCO ) kuna upotevu wa fedha za wakulima billion 123  kupitia AMCOS hivyo wale wote waliohusika lazima watachukuliwa  hatua " alisema Bashe.

Pia aliitaka bodi ya pamba nchini kujizatiti na kuimarisha ushirika ili mkulima aweze kuzalisha zao hilo kwa bei ndogo ili aweze kupata tija ya kilimo hicho kwani sekta ya pamba ni nzuri kama utakuwepo muungano wa ushirika utakaofanya mageuzi makubwa hivyo serikali inalenga kuwekeza katika uzalishaji wa mbegu.

Alisema kilimo ni biashara hivyo ni vyema misingi yake iheshimiwe suala la mbegu tayari linashughulikiwa lakini serikali haitakuwa tayari kupewa masharti yasiyokuwa na maslahii kwa Taifa kutoka kwa wafadhili wa nje.

" Serikali itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuwajengea njia nzuri ili wasipate hasara na haitaingilia suala ya bei ya pamba ila soko ndio litakaloamua " alisema Bashe.

Aliongeza kuwa mkopo wa mabenki nchini ni Trillion 16 asilimia nane tu ndiyo inaenda kwenye kilimo, pia sekta ya kilimo haikopesheki kutokana kutokuwa na dhamana hivyo serikali imeamua kutafuta fedha na kuipatia benki ya maendeleo ya kilimo  (TADB) ili ichukuwe dhamana ya kuwakopesha wakulima na imeanza mazungumzo na taasisi za kifedha za kimataifa zitakazoipatia fedha benki hiyo ili iwe na uwezo wa kukopesha wakulima ambapo hivi sasa washapatiwa billion 40.

Awali ya yote akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano huo wenye kauli mbiu ya wekeza kwenye tija kuongeza kipato cha mkulima na kufikia uchumi wa viwanda Mwenyekiti wa balaza la wakurugenzi bodi ya pamba Joe Kabisa alisema hatari iliyopo sasa katika kilimo cha zao hilo ni uwepo wa funza wekundu hivyo harakati za haraka zinaitajika ili kuwadhibiti ili kuwa na maendeleo endelevu ya sekta hiyo nchini.

Aliongeza kuwa kutokuaminiana ndani ya sekta ni changamoto kubwa inayowakabili hivyo ushirikiano wahitajika ili kusonga mbele pia alimuomba Naibu waziri Bashe kuimarisha mfuko wa pamba unaowezesha upatikanaji wa pembejeo.

Naye Mkurugenzi wa bodi ya pamba Marco Mtunga alisema changamoto muhimu zinazolikabili zao la pamba ni kukosekana kwa uhakika wa upatikanaji wa pembejeo bora zikiwemo mbegu, viuatilifu, mbolea vinyunyizi, utoaji hafifu wa huduma za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo hivyo vinachangia tija duni na ubora hafifu.

Dkt Charles Tizeba aliyekuwa Waziri wa Kilimo , Umwagiliaji na Ushirika, Agrey Mwanri Mkuu wa Mkoa wa Tabora na  Mohammed Yahaya Mkulima ni baadhi ya washiriki wa mkutano huo walisema elimu inayohitajika na yenye maslah kwa taifa ni ya uzalishaji wa zao la pamba .

Pia  ili kuwa na uendelevu wa uzalishaji , serikali iachie mazao makubwa likiwemo zao la pamba yajiendeshe pasipo kutegemea ruzuku ya serikali.

" Uboreshwaji wa viuatilifu uzingatiwe kwa sababu imegeuka changamoto kwa sisi wakulima tunapulizia kwenye mazao yetu lakini mdudu asife na kusababisha tupate hasara"alisema Yahaya.





Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti