• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wanafunzi wakutanishwa kufanya mitihani ya kujiandaa

Posted on: August 28th, 2019


Siku chache baada ya Serikali mkoani Mwanza kuweka maazimio 14 kwa  walimu wakuu, maofisa  elimu wa kata na taaluma ili kuinua ufaulu kwa shule za msingi 2019/2020, imeanza kutekeleza kwa vitendo kwa wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa Taifa kati ya Septemba 11-12, mwaka huu.

Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Michael Ligola kwa kushirikiana na maafisa elimu taaluma wa wilaya wamelazimika kutunga mtihani unaoelekeana na ule wa taifa na kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali katika kituo kimoja ili kujipima.

Zoezi hilo limeanza ambapo baadhi ya  shule kutoka Jiji la Mwanza na Ilemela zimekutanishwa pamoja  katika Shule ya Msingi Nyanza  na kupatiwa mtihani wa kujipima kwa kufuata muda na masharti yale yale yanayokuwepo katika mtihani wa kitaifa, ambapo shule itakayoifaulisha wanafunzi wengi itakabidhiwa fedha taslimu na  mbuzi kwa ajili ya mahafali.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Ligola, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mwanza, Longino Ludovick alisema lengo la Serikali ya mkoa ni kuhamasisha, kuboresha taaluma na kuwaandaa wanafunzi   kuelekea mtihani wa taifa unaotarajia kufanyika Septemba 11 na 12, mwaka huu.

Amwongeza  kuwa kwa  wiki mbili zilizobaki wataendelea na zoezi hilo kwa shule mbalimbali ambapo changamoto zitakazokuwa zikionekana kwa wanafunzi zitatafutiwa majibu haraka kwa kipindi kilichobaki huku akianisha kwamba zawadi zitaanza kutolewa Agosti 30, mwaka huu.


“Leo  kama unavyoshuhudia  tumezikutanisha shule nne ambazo ni Butimba A na B, Bwiru na Gedeli ambazo zimetoka Ilemela na Jiji la Mwanza, hizi shule tumezikutanisha kwa sababu katika mtihani wa Mock zilifanya vizuri hivyo tunataka kuona ipi inaongoza, shule itakayofaulisha wanafunzi wengi watapata zawadi ya pesa na mbuzi  kwa ajili ya kitoweo cha mahafali.


“Kwa wiki moja au mbili zilizobaki tutaendelea katika shule zingine na changamoto zitakazojitokeza tutazifanyia kazi haraka kabla ya mtihani wa taifa, mitihani hii imetungwa na jopo la maofisa elimu kutoka mkoani na wilayani ndio maana unatuona hapa tukishughulika katika kituo hiki cha Shule ya Msingi Nyanza".


Teleza Deus kutoka Shule ya Msingi Gedeli alisema maswali ya somo la Kiingereza waliyopatiwa ni marahisi ambapo aliahidi kupata 45 kwa 50  huku akifafanua kuwa walimu wao wamekuwa wakiwapa majaribio kila ijumaa, hivyo haoni shida kufaulu au shule yao kuibuka kidedea.


Naye Jovin Msiba kutoka Shule ya Msingi Bwiru alisema mtihani huo wa Kiingereza ni kawaida na maswali mengi aliyokutana nayo amefundishwa na walimu. Aliongeza kuwa walimu wao wamekuwa wakiwapatia majaribio  ya kujipima kila wiki ambapo maswali mengi alikuwa anayajua.


Hata hivyo wanafunzi wengine, Julius William na Vailet Javis kutoka Butimba A na B walitamba kwamba shule yao itaibuka kidedea kwani  maswali mengi wamejifunza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti