• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wataalam wa Maabara Mwanza wakumbushwa kutoa huduma bora na kuzingatia miiko ya kazi

Posted on: April 25th, 2023


Wanachama na wadau wa Chama cha  Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT) Mkoa wa Mwanza  wametakiwa kushiriki kikamilifu shughuli mbali mbali za chama kama njia ya kuendelea kudumisha huduma kwa  wananchi

Wito huo umetolewa  leo Aprili 25 2023 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana wakati akifungua Maadhimisho ya Wiki ya  Wataalam wa Maabara Mkoa wa Mwanza katika viwanja vya Furahisha Wilaya ya Ilemela.

Bw. Balandya ameongeza kuwa wadau na  wataalam wa maabara watumie maadhimisho hayo kama njia ya kuboresha huduma  katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

"Nitoe wito kwa wataalam wote wa Maabara Mkoa wa Mwanza kuwa wanachama hai wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeSALT) na kushiriki katika shughuli mbali mbali za chama pia Waajiri  mtoe ruhusa kwa Wataalam wa Maabara kushiriki shughuli za chama bila kuathiri utoaji huduma kwa wananchi," Amesema Mtendaji huyo wa Mkoa

Aidha  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuhakikisha kuwa huduma za afya zinazotolewa zinakuwa bora kwa kusimamia ubora wa huduma za maabara za Serikali na za watu binafsi.

"Mkoa wa Mwanza kupitia timu ya usimamizi wa huduma za afya  tunaendelea  kusimamia na kuhakikisha kuwa huduma zote za afya zinazotolewa zinakuwa bora kwa kusimamia ubora wa huduma za maabara za Serikali na watu binafsi," amesema Rutachunzibwa

Pia Mwenyekiti wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeSALT)  Bertrand Msemwa amesema anaiomba serikali kuendelea kuajiri wataalam wa Maabara ili waweze kufanya kazi katika kiwango ambacho kinatakiwa na huduma ziweze kutolewa nzuri.

Naye Katibu wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT) Mkoa wa Mwanza Bw. Yusuphu Mkama amesema  wananchi wa Mkoa wa Mwanza  wafike sehemu maadhimisho yanapofanyika ili waweze kupatiwa huduma  za vipimo bure.

"Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Mwanza muweze kufika mahali hapa ambapo maadhimisho yanafanyika muweze kupatiwa huduma na kujua afya zenu kwakuwa huduma za vipimo ni bure,"amesisitiza Mkama

Maadhimisho hayo yamefanyika Ki- Mkoa kwa mara ya 2 ikiwa ni maadhimisho ya 12 tangu kuanzishwa ambayo yanafanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia Aprili 24  hadi Aprili 28 2023.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti