• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Watano wakamatwa mauaji ya Albino Kwimba,Mwanza

Posted on: November 9th, 2022


Watu watano wakamatwa wakituhumiwa kuhusika na Kifo cha kikatili cha Ndugu Joseph Mathias (28) kilichotokea usiku wa tarehe 02 Novemba, 2022 kwa kukatwa Mkono wa kulia na kusababisha kifo chake katika kijiji cha Ngulla wilayani Kwimba.

Hayo yamebainishwa na Mhe. Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya kuwasaka watuhumiwa wa sakata hilo ambao wamekamatwa kwenye maeneo wilayani Misungwi.

"Wiki iliyopita yalitokea mauaji mabaya sana na nilitoa maagizo kwa jeshi la Polisi na vyombo vingine vinavyohusika na uchunguzi kuhakikisha wanawakamata watu wote waliohusika na tukio hilo na juzi wamewakamata wahalifu hao, kwakweli nawapongeza sana Jeshi la Polisi na wananchi wote waliotoa ushirikiano." Amesema Mhe. Malima.

Amefafanua kuwa Marehemu Mathias amefikwa na umaiti kutokana na kupoteza damu nyingi kwani pale nyumbani kwake alikatwa mkono kwa kutumia kitu kikali na marehemu alibaki akihangaika pale na akapoteza damu nyingi sana.

Vilevile, ametoa agizo kwa vyombo vinavyohusika na Uchunguzi kuendelea kufuatilia mwenendo mzima wa uovu huo ili asibaki hata mtu mmoja aliyehusika bila kukamatwa aidha awe aliyetekeleza mauaji, aliyetengeneza mazingira, mwendesha bodaboda aliyewabeba, Mganga wa kienyeji au hata mwanasiasa yeyote kama alihusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa SACP Wilbroad Mtafungwa amefafanua kuwa Marehemu Joseph Mathias aliuawa usiku wa tarehe 02 Novemba 2022 na watu waliofika nyumbani kwake na kumwita atoke nje na alipotoka alishambuliwa na takribani watu wapatao watano na kumkata Mkono na kuondoka nao na kusababisha kifo chake kwa kupoteza damu.

Ameongeza kuwa Jeshi la polisi limefanya Msako mkali kwenye maeneo mbalimbali wilayani Kwimba na siku ya Tarehe 06 Novemba, 2022 walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyebeba begi jeusi na baada ya upekuzi alikutwa na Mkono wa binadamu na mtuhumiwa alikiri kuhusika kwa kushirikiana na wenzake kufanikisha uovu huo.

"Baada ya Uchunguzi wa Kitaalamu imebainika ya kwamba Mkono ule ni wa Marehemu Joseph Mathias na Mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake tunaendelea kuwahoji na kwa hakika msako mkali unaendelea na kwamba hatobaki mtu hata mmoja ambaye amehusika na mauaji hayo na baadae watafikishwa mahakamani." Kamanda Mtafungwa.

Kamanda Mtafungwa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuliamini jeshi la polisi na kusaidia kufanikisha kuwakamata wahalifu na pia ametoa onyo kali kwa jamii kuacha mara moja kufanya vitendo vya kihalifu kwani watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti