• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Watanzania wapewa Rai ya kuuenzi Muungano kwa kufanya kazi

Posted on: April 26th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhe. Adam  Malima amewasihi Watanzania kuuenzi muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutobaguana na kuuchukulia Muungano  kama nguzo ya mafanikio na kufanya kazi kwa bidii

Mhe. Malima amesema hayo leo Aprili 26 2023 katika Maadhimisho ya Miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo ki mkoa  yamefanyika katika wilaya ya Kwimba na kuongoza uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kwenye Chuo cha ufundi Veta ambapo Mkoa wa Mwanza umejipanga kupanda miti milioni 23

"Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta mambo mengi ya kimaendeleo na waasisi wetu walituasa Muungano uende pamoja na kufanya kazi ili kulijenga Taifa letu," Amesema Mhe. Malima

Mbali ya zoezi hilo la upandaji miti,Mhe. Malima katika kutekeleza azma ya Muungano ni kazi ya kuijenga nchi,amezindua  mradi wa maji kwenye Kijiji cha Malembe kata ya Igongwa Wilayani Kwimba iliyogharimu zaidi ya Shs milioni 900  na kuwataka wananchi kuilinda miradi hiyo kwa faida ya vizazi vijavyo.

" Naishukuru Serikali hii ya awamu ya sita imeonesha kutujali wananchi wa Mwanza kwa kutupatia miradi ya kimkakati ambayo inachochea maendeleo katika mkoa wetu,". Amesema Mkuu huyo wa Mkoa

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu  Ludigija amesema wanajivunia na kuishukuru serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea fedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli za  kijamii

" Wananchi wa Kwimba na maeneo ya jirani tunaishukuru na tunajivunia miundombinu na uwekezaji mkubwa ambao Rais wetu ameufanya kwenye Wilaya yetu ya Kwimba kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kijamii,". Amesema Mhe. Ludigija

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa ametumia maadhimisho hayo kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa chanjo na kuwahamasisha  kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata huduma hiyo.

" Nitoe rai kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanapelekwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuhakikisha  wanajikinga na magonjwa,". Amesema Dkt. Rutachunzibwa

Tanzania huadhimisha Sherehe za Muungano kila ifikapo Aprili 26 huku Watanzania wakifanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa kama ishara ya kuuenzi Muungano huo uliofanywa na waasisi wetu Mwl Julius Nyerere na Abeid Karume Aprili 26,1964.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti