• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wavuvi Kisiwa Cha Ghana Ukerewe kunufaika punguzo la tozo ushuru wa mazao ya samaki

Posted on: September 26th, 2020

Wavuvi wamehakikishiwa punguzo la tozo, ushuru wa mazao ya samaki na  kodi kwenye zana za uvuvi waweze kunufaika.

Unafuu huo utapatikana baada ya  mabadiliko ya sheria yatakapofanyika  ili waweze kupata fursa ya kufanya biashara na kujipatia mapato .

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi  wa kisiwa kidogo  Gana kata ya Ilangala wilaya ya Ukerewe kwenye mkutano wa kampeni za mgombea  Urais wa CCM, Dkt. John Magufuli.

Alisema wilaya ya Ukerewe asilimia 90 ya wakazi wake ni wavuvi hivyo serikali itaimarisha maeneo ya uvuvi kwa kupunguz ushuru wa samaki ambao kwa sasa ni sh. 300 ambayo wavuvi wameomba ifishuke na kubaki sh.100.

Alisema ushuru wa dagaa ni sh .100 kwa sasa lakini wameomba punguzo la sh.50  hivyo serikali yao imewasikiliza na inakwenda kubadilisha sheria ili wafanye biashara vizuri na kukuza vipato vyao.

Aliwaasa wavuvi kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaimarisha sheria na kubadilisha maeneo yote yenye kero .

Akizungumza suala la kodi alisema wanaendelea kuodoa kodi zote hasa kwenye zana za uvuvi ,kuwaondolea ada ya leseni ya kuuza na kuvua samaki Ziwa Victoria watokanao na maji baridi, pia mchakato wa kuimarisha upatikanaji wa nyavu kwenye maduka unaendelea ili kuwasogezea huduma.

Kwenye kuondoa kodi tumeanzia kwenye  vyavu,nyuzi zinazoshona  nyavu, engine (mashine za kuoachika) zinazobebwa mkononi na kuwekwa kwenye mitumbwi,vifungashio kwa watu wa viwanda tunaendelea suala la upatikanaji wa nyavu kama kuna tajiri yeyote yupo huku hiyo ndio fursa anzisha duka la kuuza bidhaa za uvuvi na wewe tutakupunguzia kodi ,endeleeni kuiunga mkono serikali yenu na sisi hatutawaangusha"alieleza Majaliwa.

Aliongeza kuwa sekta ya Uvuvi imeimarishwa kwani huko nyuma walikuwa na migogoro , Ziwa Victoria linavuliwa na nchi tatu huku wavuvi wa nchi hizo wakituhumiwa kuwanyanganya samaki ,hatuwazuii lakini watuachie kila mmoja aende upande wake hivyo zoezi lile lilikuwa la kuwekana sawa,kutambuana ili wapangane vizuri na walifanikiwa.

Aliongeza kuwa wataleta boti kwa ajili ya makamanda ili kuimarisha ulinzi kwa wavuvi wakiwa ziwani Baada ya kukubwa na matukio ya wavuvi kutoka nchi zingine kuwavamia na kuwanyanganya bidhaa zao ,hivyo makamanda 67 wa maji watakuwa wanafanya kazi ulinzi.

" Zamani Wizara hii ilikuwa kubwa mno ilikuwa Kilimo, Mifugo na Uvuvi lakini Mhe. Dkt.John Magufuli ameitenga sasa ipo ya Uvuvi na Mifugo tu mambo yamekwenda kuratibiwa na tumeanza kukaa na wavuvi ili kurekebisha sekta hii tunachofanya sasa tunaunga makundi ya wavuvi ili kuweza kuwafikia tuweze kuyasikia matatizo yenu pia kazi tunayoifanya Sasa waziri wetu anapita kukutana na wavuvi kusikiliza na kuchukua changamoto zao ili ziweze kutatuliwa" alieleza Majaliwa.

Pia akizungumzia suala la vivuko alisema   wanafufua meli zote za zamani ambazo zinakarabatiwa ili zifanye kazi hasa maeneo ya visiwani pia uimarishwaji  na uboreshwaji wa vivuko unaendelea ,kukamilisha ujenzi wa vivuko vyote  sambamba na ujenzi wa meli mpya kubwa ambayo inatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200,tani 400 za mizigo .

Pia Majaliwa alitoa ahadi ya kuwatatulia changamoto ya umeme,maji ,afya  ,elimu pamoja na kufanya ukarabati wa shule,ujenzi wa mabweni na kuifanya ghana kuwa hadhi ya Kijiji kutoka kitongoji sambamba na kuwajengea Zahanati  ili wananchi hao waweze kupata huduma hivyo wakichague chama cha mapinduzi  kwani ndiyo yenye kuwaletea maendeleo zaidi .

" Tukishamaliza hizi pilikapilika ziara yangu ya kwanza itakuwa Ilugwa na Ghana kwani ndani ya miaka mitano nimeweza kufika huku pia mtambue kuwa mnayo haki ya kuchagua viongozi imara wenye uwezo wa kuongoza na kuisimamia serikali,  tuna mambo mengi  tumeyafanya lakini tunataka kuboresha zaidi."alieleza Mhe.Majaliwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti