• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Wananchi wa eneo la Fela kupimiwa viwanja ili kunufaika na mradi wa SGR

Posted on: October 16th, 2022


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Misungwi  mkoani Mwanza  Benson Mihayo

 kupima viwanja eneo la Fela ili wananchi  waweze kunufaika na uwepo wa bandari kavu inayotarajiwa kujengwa katika  eneo hilo.

Mhe. Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2022 akiwa eneo la Fela  Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza   baada ya kukagua maendeleo ya  ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) kipande kinachoanzia Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa kilomita 341 kinachojengwa kwa gharama ya Shilingi Trilioni 3.06 .

Amesema viwanja vilivyopo eneo hilo vikipimwa vitawanufaisha wananchi kwani wenye uwezo wa kifedha wataweza kujengwa hoteli na nyumba  za kulala wageni hivyo kujiongezea kipato wao na Taifa kwa jumla.

Aidha, Mhe. Majaliwa amewataka watanzania waliopata nafasi ya kuajiriwa kwenye mradi huo kufanya kazi kwa weledi na bidii huku wakizingatia mafunzo wanayoyapata  maana Serikali inawategemea kwa ajili ya kuteleleza miradi mingine.

"Mkifanya kazi kwa weledi nawahakikishia mtaisaidia sana Serikali maana ujuzi mnaoupata kutoka kwa wakandarasi wageni wakiondoka tukianzisha miradi mingine Serikali itawatumia nyie hivyo tutapunguza gharama za kuleta wataalamu wa kigeni kutoka nje ya nchi,"ameongeza.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema mradi huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 14.12 ni mhimili mkubwa na thabiti katika ukuaji wa uchumi wa taifa maana ukikamilika  utaleta mapinduzi katika sekta za viwanda, kilimo, ujenzi, ufugaji, usafirishaji, madini pamoja na utalii.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Amina Lumuli amebainisha kwamba mradi huo umekuwa na mafanikio mengi kwa watanzania kwani hadi Septemba 30, 2022 ulikuwa na jumla ya wafanyakazi 5,897 kati ya hao 5,384 sawa  na asilimia 91.3 ni watanzania na 513 sawa na asilimia 8.7 ni raia wa kigeni.

Ameongeza kuwa TRC imeendelea kutoa mafunzo ya  vitendo kwa wataalamu wake mbalimbali, mafunzo hayo yamekuwa na tija sana kwani zaidi ya wataalamu 40 wanashiriki moja kwa moja kwenye ujenzi wa mradi wa  SGR.

" Mradi huu ukikamilika utakuwa na faida mbalimbali ikiwemo kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari mathalani kutoka jijini Dar es Salaam  hadi Mwanza kutoka masaa 18 hadi 20 ya awali hadi nane, vilevile  utachochea uanzishwaji  wa miji midogo katika sehemu zinazojengwa stesheni ambazo zitakuwa kivutio kwa wananchi.

" Pia utapunguza  gharama za usafirishaji mizigo kati ya asilimia 30 hadi 40  na kuifanya bandari ya Dar es Salaam kuhimili ushindani, utachochea uanzishwaji wa viwanda maeneo mengine ya nchi kutokana na uwepo wa uhakika wa usafirishaji wa malighafi na bidhaa,"ameeleza.

Mhe. Majaliwa yuko Mkoani Mwanza  tangu Oktoba 15 ,2022, kwa ziara ya siku nne ya kikazi lengo likiwa ni kukagua maendeleo ya miradi ya  kimkakati inayotekelezwa na Serikali pamoja na kukutana na wananchi ili kuwaeleza kuhusu  miradi  mbalimbali ambayo serikali ya awamu ya sita inaitekeleza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti