• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu Majaliwa aridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Daraja la JP Magufuli

Posted on: October 16th, 2022


Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa ameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la J.P.Magufuli ( Kigongo Busisi ) na kuwahakikishia wananchi kwamba daraja hilo litakamilika kama ilivyopangwa kufikia Februari 2024 kutokana na daraja hilo kufikia asilimia 54 ya utekelezaji wake.

Mhe. Majaliwa amesema hayo mara baada ya kuwasili eneo la Busisi alipokuwa akizungumza na wananchi na kuwaeleza kuwa ameanza Ziara yake kwa kukagua Daraja la J.P. Magufuli (Kigogo - Busisi) lenye urefu wa kilomita 3.2 na barabara unganishi kilomita 1.66,linalosimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

"Miradi yote waliyoianzisha hakuna mradi utakwama, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mama Samia ambaye alikuwa Makamu wake na mimi pia nilikuwepo na Mama Samia sasa ni Rais kamili na mimi  namsaidia Mhe.Rais Samia hakuna kitu kitakwama," amesema Mhe.Majaliwa.

Aidha, Mhe, Majaliwa amewataka wananchi kuendeleza ushirikiano wa kutunza miundombinu na vifaa vinavyotumika katika daraja hilo kwani kwa kufanya hivyo zitatumika fedha zilizopangwa bila kuongeza nyingine.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya Mradi huo  Mhandisi Paschal Ambrose  amesema hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi Bilioni 716.333 ikiwa inajumuisha Mkandarasi Shilingi Bilioni 699.278, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa Ujenzi Shilingi Bilioni 11.106, pamoja na fidia Bilioni 3.145 na Usanifu Bilioni 2.803.

Ameongeza kuwa, hadi sasa Mradi umetoa jumla ya ajira 864, kati ya hizo ajira 809 sawa na asilimia 93.63 zimetolewa kwa Watanzania na ajira 55 sawa na asilimia 6.37 ni za wageni na kubainisha kuwa unazingatia Jinsia kwani asilimia 2.31 ya wafanyakazi wote ni wanawake.

"Mradi huu unatumika kama sehemu ya mafunzo kwa kada za Kihandisi, hadi sasa kuna jumla ya Wahandisi 12 wanaopata mafunzo kwa vitendo, kati ya hao 3 wanatoka TANROADS na 9 ni wale waliopita kwenye Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na yataendelea kuwa endelevu na tunategemea hadi kukamilika kwa Mradi huu Wahandisi wa kutosha watakuwa wamejengewa uwezo na ujuzi kwa ajili ya kusaidia Taifa," amesema Mhandisi Ambrose.

"Daraja hili litakuwa kiungo muhimu kati ya Mikoa ya Mwanza, na Mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa pia Nchi za jirani za Rwanda, Burundi,na Uganda na litakuwa kichocheo kikubwa cha kupunguza umaskini na kuhakikisha ukuaji wa uchumi katika eneo la Kanda ya Ziwa na Nchi za Maziwa makuu pamoja na kuondoa msongamano wa magari uliokuwa unatokea kwa wavukaji na kupunguza muda wa kusafiri," ameongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amesema amefarijika sana na ujio wa ugeni huo kwani ni baraka na faraja kwa wananchi wa Mwanza na kumuomba Mhe.Waziri Mkuu kufikisha salamu za Shukurani za wanamwanza kwa Mhe.Rais.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo ya kimkakati iliyopo Mkoa huo.

Mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na upo chini ya Mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation  akishirikiana na China Railway 15 Bureau Group Cooperation (CCECC -CR15GJV  zote za China ambapo utekelezaji kwa ujumla umefikia asilimia 54 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 24,2024

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti