• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

WEKEZENI KATIKA MICHEZO NI AJIRA YA UHAKIKA KWA WANAMICHEZO-RC MAKALLA

Posted on: July 28th, 2023

WEKEZENI KATIKA MICHEZO NI AJIRA YA UHAKIKA KWA WANAMICHEZO-RC MAKALLA


*Awashauri wenye shule kuvibaini vipaji na kuweka mikakati ya kuviendeleza


*Asema wanamichezo sasa ndiyo wanaotamba Duniani kwa kupata vipato vikubwa


Wamiliki wa shule na wadau wa michezo kwa ujumla Mkoani Mwanza wameshauriwa kufanya uwekezaji wa kweli katika sekta ya michezo kwa kuvibaini vipaji na kuweka mikakati ya kuviendeleza.

Akizungumza Alhamisi hii kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana mara baada ya mchezo wa fainali soka la wanawake  ligi ya mabingwa mkoa ngazi ya Taifa kati ya Fountain Gate na Mwanga FC,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla amesema mafanikio katika michezo ni matokeo ya uwekezaji mzuri kwa kuvibaini vipaji vya wachezaji tangu hatua za awali.

Makalla ambaye amesakata kabumbu miaka ya nyuma amebainisha Ulimwemguni hivi sasa wanaotamba kwa vipato vikubwa ni wanamichezo mbalimbali ambao ni matunda ya kuandaliwa tangu wakiwa na umri mdogo.

"Tumeshuhudia mchezo mzuri wa fainali soka la wanawake umri wa wachezaji hawa ndiyo sahihi kuhakikisha wanawekewa mikakati kamambe ya kuendelezwa,mwanangu kasoma shule hii ya Fountain Gate sasa hivi yupo kwenye majaribio huko Hispania," amefafanua CPA Makalla

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mpambano huo wa fainali, amewapongeza mabingwa wa michuano hiyo timu ya Fountain Gate kutoka Dodoma kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwanga ya Kigoma,matokeo ambayo yamewapa tiketi ya kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Michuano hiyo ya Ligi ya mabingwa mkoa kwa upande wa wanawake ngazi ya Taifa,imeshirikisha jumla ya Mikoa 19 huku michezo hiyo  ikirindima kwenye viwanja vya Nyamagana na CCM Kirumba.

Miongoni mwa mashuhuda wa mchezo huo wa fainali ni pamoja na Rais wa Shirikisho la soka nchini,TFF Wallace Karia,Mwenyeki wa kamati ya soka la Wanawake nchini,Hawa Mniga, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mwanza,MZFA Vedasto Lufano na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti