• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

ZIARA YA RC MTANDA HOSPITALI YA JESHI YAWAIBUA WANANCHI, WAFIKA KUPATA HUDUMA ZA KIBINGWA

Posted on: June 4th, 2024

ZIARA YA RC MTANDA HOSPITALI YA JESHI YAWAIBUA WANANCHI, WAFIKA KUPATA HUDUMA ZA KIBINGWA


Kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda aliyoifanya Mei 24, 2024 kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Hospitali ya Kanda ya Jeshi la Wananchi Mwanza iliyopo wilayani Ilemela, wananchi waanza kufika ili kupata matibabu ya kibingwa na kupongeza kwa huduma nzuri.

Hayo yamedhihirika baada ya Bi. Dina Mgeta kutoka Mkoani Mara kufika kwenye hospitali hiyo mnamo Mei 31, 2024 akiwa na uvimbe usio wa kawaida shingoni ili kupata matibabu ambapo leo Juni 04, 2024 mgonjwa huyo amezungumzia furaha yake baada ya kufanyiwa upasuaji wenye mafanikio na hali yake kuwa nzuri.

Mgonjwa huyo amemshukuru Mkuu wa Hospitali hiyo kwa ukarimu na moyo wa kiungwana kwani mara tu baada ya kumpokea alihakikisha anamhudumia hata baada ya kubaini kuwa mgonjwa huyo aliyeletwa na mama yake mzazi kutokua na fedha za matibabu wala bima ya afya hivyo kulazimika kuomba kupatiwa matibabu kwa msamaha.

Mgonjwa huyo ameonesha furaha yake kutokana na kupata matibabu mazuri ya kibingwa na akatumia wasaa huo kutoa wito kwa wananchi wengine kuhakikisha wanakata Bima ya Afya kwani inasaidia sana endapo unapata maradhi na kuhitaji matibabu jambo ambalo yeye alishindwa kufanikisha kutokana na kukosa bima.

Mkuu wa Hospitali ya Kanda ya Jeshi Mwanza ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji na ndiye aliyemfanyia Upasuaji mgonjwa huyo, Luteni Kanali Ahmed Shabhay amesema walimpokea mama huyo akiwa na uvimbe mkubwa shingoni (Huge Multi-nodular Goiter) na alihitajika kufanyiwa upasuaji wa kutoa uvimbe huo.


Amesema, Mama huyo hakuwa na fedha za matibabu na wala hakua mnufaika wa bima ya afya na aliifikisha changamoto yake kwenye uongozi wa hospitali nao kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa walifanikisha na kumfanyia upasuaji Mei 31,2024 ambao umeenda salama kutokana na vifaa tiba na wataalamu tiba na kwamba kwa sasa yupo salama na ameruhusiwa kwenda nyumbani kwani matibabu hayo yamekamilika.

Luteni Kanali Ahmed Shabhay ametoa wito kwa wananchi kutoka Mwanza na mikoa ya jirani kufika kwenye hospitali hiyo kupata matibabu ya kibingwa kwani wana watoa huduma wabobevu na vifaa vya Kisasa na kwamba wanahudumia Maafisa, Askari na familia zao pamoja na raia kwa njia zote za malipo ya papo kwa papo na Bima ya afya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti