BILIONI 7.2 KUJENGA MABWENI TIA KAMPASI YA MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amewataka wananchi wa Mtaa wa Nyanghomango kulinda miundombinu ya mabweni ya wanafunzi katika taasisi ya uhasibu Tanzania tawi la Mwanza.
Amezungumza hayo leo Oktoba 17, 2024 wakati wa hafla ya kukabidhiana hati za ujenzi wa mabweni mawili baina ya kampuni ya Wakandarasi wa CAIEC na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.2 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 306 wa kike pamoja na kiume.
Vile vile Mhe. Samizi ameishukuru serikali kwa kuunufaisha Mkoa wa Mwanza kwa miradi ya elimu huku akiwataka wakandarasi kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wa karibu na eneo la mradi.
"Tunafahamu hizi kazi zinahitaji taaluma lakini zile kazi ambazo hazina ujuzi tuwaangalie watu wa eneo hili ili hizi pesa zinazopatikana katika mradi huu ziweze kuwanufaisha nawao". Amesema Mhe. Samizi.
Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa. William Pallangyo amemtaka mkandarasi anaesimamia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya miezi 18 ya mkataba huku akiwaahidi ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha ujenzi huo.
"Tutahakikisha tunawalipa ndani ya muda na tutahakikisha tunawapa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha mradi unaaga dunia". Amesema Prof. Pallangyo.
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya CAIEC inayotekeleza mradi huo Ndg. George Moses amesema kampuni yao itakamilisha mradi kwa wakati na wananchi wanaoishi karibu na mradi watanufaika na fursa zitakazojitikeza katika mradi huo.
Mradi huo wa ujenzi wa mabweni unatekelezwa na fedha za mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.