BODABODA MWANZA WASEMA HAWATAANDAMANA JANUARI 24
*Wasema shughuli yao inawapatia fedha za kuendesha familia na uchumi*
*Wasema hawataki madhara yatokanayo na maandamano*
*Wamshukuru Rais Samia kwa kuboresha barabara kupitia TARURA*
*Waishukuru Serikali kwa kupunguza faini ya adhabu kutoka elfu 30 hadi elfu 10*
Mwenyekiti wa Chama cha waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Mwanza Makoye John amesema Jumuiya hiyo inalaani vikali maandamano yaliyopangwa na vyama vya upinzani kwamba yatafanyika kwenye sehemu mbalimbali nchini Januari 24, 2024.
Ametoa kauli hiyo mapema leo Januari 20, 2024 jijini Mwanza wakati wa mkutano wa umoja wa Jumuiya hiyo na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye viwanja vya Jiwe la Bismark ulio kwenye fukwe za ziwa victoria.
Amesema, shughuli yao inayowajumuisha zaidi ya wanachama 230,000 inawaingizia kipato na kuimarisha uchumi wao na kwamba hawako tayari kuathiri shughuli yao yenye tija kwa kujihusisha na maandamano ambayo yana athari kubwa kwenye amani.
"Mwanza hakuna matukio ya uvunjifu wa amani, sisi kama chama halali kilichosajiliwa na kufuata miongozo ya Wizara ya Mambo ya ndani hatupo tayari kuingia kwenye maandamano kwani tunajua madhara yake." Amesisitiza Mwenyekiti.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Joseph Msabila amesema hawatoshirki maandambano kwa maslahi ya wanasiasa wala kwa kushawishiwa na mtu na kwamba wataendelea na shughuli yao halali kwa maslahi ya familia na Taifa zima.
Mhamasishaji Abdalah Mzamiru ametumia wasaa huo kumshukuru Rais Samia kwa kupunguza faini ya makosa ya adhabu kutoka elfu 30 hadi elfu 10 na kutengeneza barabara kupitia TARURA na TANROADS kwani zinawapa usalama vya vyombo vyao na mazingira rafiki ya usafirishaji abiria.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.