CCM YAKAGUA MIRADI YA THAMANI YA SHS BILIONI 66 YAKAGULIWA NYAMAGANA
Miradi 5 yenye thamani ya shs bilioni 66 imekaguliwa leo Mei 27,2024 Wilayani Nyamagana na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoani Mwanza na kuridhiwhwa na thamani ya fedha ilivyotumika.
Miongoni mwa miradi iliyowafurahisha wajumbe wa Kamati hiyo ni ule wa chanzo cha maji Butimba ulio kwenye hatua ya maboresho baada ya ujenzi kukamilika uliogharimu shs bilioni 71.
"Kaimu Mkurugenzi wa MWAUWASA kwa niaba ya wajumbe wenzangu nakupa pongezi sana kwa kukamilisha mradi huu mkubwa tena wa kisasa unaokwenda kuwaondolea usumbufu wa ukosefu wa maji wakazi wa Mwanza," Mhe. Michael Lushinge,M/kiti CCM Mkoa.
Mhe. Lushinge amesema maji ni rasilimali muhimu sana katika maisha ya kila siku, amesikia mikakati mizuri inayofuata kuhakikisha huduma hii inawafikia wengi hatua ambayo imefuata ilani ya CCM inavyoelekeza.
"Mhe. Mwenyekiti mradi huu tunatarajia kukabidhiwa rasmi Disemba mwaka huu, na tupo mbioni kuingia mkataba wa ujenzi wa Matenki makubwa 5 yenye ujazo wa lita milioni 10 yatakayojengwa maeneo ya Buhongwa na Fumagila,"Nelly Msuya,K/Mkurugenzi MWAUWASA.
Kamati hiyo ikiwa kwenye Kituo cha afya Mkolani imeshuhudia upanuzi wa kituo hicho uliogharimu shs milioni 848 ujenzi uliofanywa mwaka 2022 na kukamilika 2023 na sasa kukidhi kuwahudumia wateja wengi zaidi kutoka kata ya Mkolani na Nyegezi
"Kituo hiki cha afya kimegharamiwa na Halmashauri ya Jiji shs mil 300 kutokana na mapato ya ndani na shs milioni 548 zimetoka Serikali kuu,"Dkt.Pima Sebastian.
Miradi mingine iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni Soko kuu la mjini kati lenye gharama ya shs bilioni 23,upanuzi wa Ghati bandari ya Mwanza Kaskazini unaogharimu shs bilioni 18.6 pamoja na mradi wa barabara ya Buhongwa hadi Kishiri yenye urefu wa KM 14 inayojengwa na mkandarasi Zong Mein kutoka China kwa shs bilioni 22.7.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.