Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima amewataka viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuwa wabunifu ili kuongeza wigo wa Ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwa kuzingatia asili na aina ya vyanzo vilivyopo ili kuwa na uwezo mkubwa wa hudumia wananchi.
Ametoa agizo hilo leo Agosti 04, 2022 wakati akizungumza na viongozi, watumishi na wadau wa maendeleo wilayani humo alipofika akiwa katika ziara ya kujitambulisha na kupata taarifa ya Maendeleo.
"Mnapopata nafasi ya kutumikia wananchi kwenye wilaya kama hii mjue mna dhamana kubwa kutokana na ukubwa wa vyanzo vyenu vya mapato hivyo wanaoshughulika na Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ni lazima watafakari hizi Bilioni 13 mlizokadiria kukusanya vyanzo vyake viko wapi na mnazipataje" Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala amesema kuwa kwa kipimdi cha mwaka 2021/22 Halmashauri iIikadiria kukusanya Tshs Bilioni 9 kutoka mapato ya ndani na wamekusanya zaidi ya Tshs Bilioni 10 na kwamba mwaka 2022/23 wameweka Malengo ya kukusanya zaidi ya Tshs. Bilioni 13.
"Tunavyo vituo vya kukusanyia taka ngumu 16 katika maeneo mbalimbali na tunaendelea kuboresha huduma za Usafi na mazingira hasa kwenye maeneo ya Mji na wananchi wa eneo hili wanajihusisha na sekta ya Uvuvi ambapo tuna mialo 15 na soko la kimataifa la Mwaloni Kirumba." Mhe. Masala amefafanua.
Aidha, amebainisha kuwa uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuboresha huduma na kutatua changamoto kwenye maeneo ya kama ya Mazingira, Elimu, Afya, Ardhi na Sekta ya Miundombinu ambapo mtandao wote wa Barabara upatao Kilomita 875 unapitika.
"Ndugu zangu, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, tunachohitaji kwenye ni ushirikiano ili tusonge mbele, tuchape kazi na tuwatumikie wananchi kwa kutoa huduma zilizotukuka twende sambamba na adhma ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake." Amesema, ndugu Balandya Elikana, Katibu Tawala wa Mkoa ame
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mhandisi Modest Apolinary amemuahidi Mkuu wa Mkoa ushirikiano wa dhati na kwamba wao kama taasisi watatekeleza maelekezo yatayotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ustawi wa wananchi wa Ilemela.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.