JAJI ASINA AWATAKA MAAFISA UANDIKISHAJI-KATA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Jaji Asina Omari amewataka Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata kwenda kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kufanikisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Jaji Mhe.Asina ametoa wito huo leo Agosti 14,2024 wakati alipokuwa akizungumza kwa nyakati mbili tofauti kwenye mafunzo kwa Watendaji hao yanayofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bwiru (Kwa ngazi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela) na katika Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza (Kwa ngazi ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza).
"Mmeteuliwa na kuaminiwa kwa ajili ya kufanya kazi hii, hivyo mkafanye kazi kwa weledi na kwa nguvu na uzalendo ili zoezi hili likamilike kwa mafanikio kama lilivyopangwa" alisema Jaji Mhe.Asina.
Kabla ya Kuanza kwa mafunzo, Maafisa hao waandikishahi wasaidizi ngazi ya Kata waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa katika chama cha Siasa mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela Mhe.Juma Ondupo.
Haya yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga Kura kwa Mkoa wa Mwanza na Shinyanga ambapo unatarajia kuanza tarehe 21 Agosti, 2024 hadi tarehe 27 Agosti, 2024, huku uboreshaji huu ukibebwa na Kauli mbiu ya "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.