Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi alipokuwa katika mradi wa Shule ya Sekondari Walla akikagua ujenzi wa madarasa 5 amewataka kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuzingatia ubora katika usimamizi.
"Niwatake kuhakikisha mnazingatia ubora na thamani halisi ya miradi wakati wa ujenzi simamieni vizuri fedha za Serikali na zingatieni muda uliopangwa ili kukamilisha kwa wakati," alisema Samike.
Akiwa katika Kata ya Walla kukagua mradi wa ujenzi wa daraja, Samike amewataka wakandarasi kusimamia vizuri ili kukidhi ubora wa mradi.
"Nimerishwa na jinsi ujenzi wa daraja hili unavyoendelea Mkandarasi naomba uendelee na usimamizi mzuri ili daraja hili liwe na ubora na likamilike kwa wakati."
Katika kuhakikisha ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa Shule ya sekondari Bungulwa na vyumba 5 Shule ya Sekondari Ngulla pamoja na maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kijiji cha Isunga Kata ya Bungulwa vinakamilika Samike amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanapata vifaa kwa wakati na kupanga majengo katika mipangilio sahihi ili kutunza mazingira kwa kupanda miti ya matunda na vivuli.
Hata hivyo,Samike amefika Bugunga na kukuta ujenzi wa tanki la maji unaendelea ambapo Mhandisi amewaahidi wananchi kuwa ifikapo Desemba wananchi wa eneo hilo na maeneo ya jirani watapata maji safi na salama.
" Nitarudi Desemba ili kujiridhisha kama wananchi wa Kata ya Malya kijiji cha Bugunga wanapata maji kama wataalamu walivyotuahidi," alisema Samike.
Aidha, amekamilisha ziara yake kwa kuongeza na watumishi wa Halmashauri hiyo na kuwasikiliza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.